member

Wednesday 12 September 2012

MACHEDA


Macheda

(Elekezwa kutoka Federico Macheda)
Macheda
Urefu6 ft 0 in (1.83 m)[1]
Playing positionStriker
Club information
Current clubManchester United
Namba27
Youth career
2006–2007Lazio
2007–2008Manchester United
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2008–Manchester United4(2)
Timu ya Taifa ya Kandanda
2006–2007Italy U-1610(2)
2007–2008Italy U-173(0)
2009–Italy U-191(0)
2009–Italy U-213(0)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 08:06, 18 August 2009 (UTC).
† Appearances (Goals).
‡ National team caps and goals correct as of 13 October 2009
Federico "Kiko" Macheda ([1] amezaliwa 22 Agosti1991) ni mwanakandanda mwenye uraia wa Kiitalia ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya Ligi kuu ya Uingereza ya Manchester United. Alijiunga na Manchester United kutokaLazio mnamo Septemba 2007.

Yaliyomo

  [ficha

[hariri]Wasifu

[hariri]Wasifu wa Klabu

[hariri]Wasifu wa Mapema

Alizaliwa katika mji mkuu wa Roma na alianza wasifu wake wa kandanda na upande wa mtaa ujulikanao kama Lazio. Hata hivyo, kutokana na kanuni za kandanda za Kiitaliano zinazowazuia wachezajji wenye umri chini ya miaka 18 kusaini mikataba ya kitaaluma, hakuwa amefungwa na klabu, na muda mfupi baada ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ya 16, alitia mkataba na klabu ya Manchester United ya Uingereza, ambapo kanuni zinaruhusu kuwasaini wachezaji wenye umri wa miaka 16 na zaidi. Kufuatia familia yake kuhamishwa kwa Uingereza, yeye alijiunga na klabu rasmi kama biträdande tarehe 16 Septemba 2007, na ilianza miaka mitatu udhamini katika klabu ya Academy.[2] aKufuatia familia yake kuhamishwa nchini Uingereza, alijiunga na klabu rasmi kama mwanafunzi tarehe 16 Septemba 2007, na ilianza udhamini wa miaka mitatu katika Academy ya klabu ya Manchester United.

[hariri]Manchester United

Alikwenda moja kwa moja kwa timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18 ya Manchester United na alifunga bao la kipekee la mechi katika mechi yake ya kwanza, ushindi wa 1-0 ugenini dhidi Barnsley tarehe 15 Septemba 2007. Katika msimu wake wa kwanza na klabu, alimaliza kama mfungaji bora wa mabao kwa timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18 ya Manchester United na jumla ya mabao 12 katika mechi 21 alizoichezea timu hiyo ya vijana na hata pia alicheza mechi yake ya kwanza kwa timu hifadhi mnamo 26 Februari 2008, wakati aliingia dakika ya 68 kama mbadala wa Gerard Pique katika kushindwa kwa 2-0 dhidi ya Liverpool. Tarehe 12 Mei 2008, Macheda alipata medali ya ushindi katika kombe la Manchester Senior alipotajwa kama mbadala ambaye hakutumiwa kwa kushinda wa 2-0 dhidi ya Bolton Wanderers kwenye fainali.
Macheda alisaini mkataba wake wa kwanza wa kitaalamu na Manchester United katika sherehe ya siku yake ya kuzliwa ya 17 mnamo Agosti 2008. Katika msimu wa 2008-09, aliendelea kushiriki katika timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 18, huku pia akiichezea timu hifadhi mechi chache. Kuelekea mwisho wa msimu, Macheda alifurahia kuichezea timu hifadhi mechi nyingi kwa kufunga mabao nane katika mechi nane, pamoja na mabao tatu katika sarea ya 3-3 dhidi ya Newcastle United tarehe 30 Machi 2009, [15] na alituzwa kwa kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kama mbadala wa timu ya kwanza katika mechi dhidi ya Aston Villa tarehe 5 Aprili 2009. Huku United ikiongozwa 2-1 na Aston Villa na ikielekea mwisho ya tatu ya mechi, meneja Alex Ferguson alimbadilisha Macheda kwa nafasi ya Nani baada ya mechi kuchezwa kwa muda wa saa moja. Baada ya Cristiano Ronaldo kusawazishia United katika dakika ya 80, Macheda aliishindia Manchester United mechi kwa mgeuko uliyomhepa difenda wake kufuatiwa na juhudi yake aliyouchonga kutoka ndani ya eneo la penalti katika dakika ya tatu muda wa ziada.
Macheda alitajwa kwenye benchi kwa mechi mbili zijazo za Manchester United - kwanza dhidi ya Porto katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, [21] na kisha dhidi ya Sunderland katika ligi – na katika mechi alicheza mechi yake ya pili kwa timu ya kwanza ya klabu. Sekunde 46 baada kuingia uwanjani kama mbadala wa Dimitar Berbatov, [23] Macheda alikuwa ameuweka mpira nyuma ya wavu kwa mara ya pili katika wasifu wake wa Manchester United, risasi yake ilimgonga kidogo Michael Carrick na kumpita mlinda lango wa Sunderland, Craig Gordon, na kuingia kwenye lango la Sunderland. Huku Alex Ferguson akiamua kuwapumzisha wachezaji wake wa majina kubwa kwa ajili ya nusu fainali ya kombe la FA Cup dhidi ya Everton mnamo 19 Aprili 2009, Macheda alianzishwa mechi yake ya kwanza kwa jezi la Manchester United. Hata hivyo, kwa mara ya kwanza katika wasifu wake wa Manchester United, alishindwa kufunga na aliondolewa kwa ajili ya Dimitar Berbatov muda wa ziada ulipoanza. Alianza mechi yake ya kwanza ya Ligi katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Middlesbrough mnamo 2 Mei 2009; yeye alihusika katika mjengo wa bao la Park Ji-Sung, lakini alishindwa kufunga bao la kibinfsi na aliondolewa dakika kumi baada ya kuanza kwa nusu ya pili. Mwishoni mwa msimu wake wa kwanza katika timu ya Manchester United ya kwanza, Macheda alitajwa kama mchezaji wa mwaka wa Jimmy Murphy Academy kama utambulisho kwa utendaje wake katika timu za vijana wasiozidi umri wa miaka 18, timu hifadhi na timu ya kwanza.
Tarehe 2 Desemba 2009, Macheda alisaini mkataba mpya wa miaka minne na Manchester United ambayo ingemfunga kwa klabu hadi Juni mwaka wa 2014.

[hariri]Wasifu wa Kimataifa

Kabla ya mashindano ya kandanda vijana wasiozidi umri wa miaka 21 ya UEFA mwaka wa 2009, Macheda alitajwa katika kikosi cha Italia cha wachezaji 40, ambao ilifaa kupunguzwa hadi wanachama 23 kwa ajili ya mashindano. Hata hivyo, Macheda alikosa nafasi na hakutajwa katika kikosi cha mwisho.
Mnamo 12 Agosti, 2009, alicheza mechi yake ya kwanza ya timu ya vijana wasiozidi umri wa miaka 21 ya Italia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Urusi.

[hariri]Takwimu ya Wasifu

KlabuMsimuLigiKombeKombe la CarlingUlayaNyinginezo [3]Jumla
MatokeoMabaoMatokeoMabaoMatokeoMabaoMatokeoMabaoMatokeoMabaoMatokeoMabao
Manchester United2008-09421000000052
2009-10000030200050
Jumla4210302000102
Takwimu sahihi tangu mechi Desemba 1, 2009. [4]

[hariri]Maisha ya Kibinafsi.

Macheda anaishi Washway Road katika sehemu ya Sale, Greater Manchester. Mapema asubuhi ya Julai 12, 2009, Macheda's nyumbani mara walengwa na wanyang'anyi, ambaye aliiba fedha taslimu na vitu vingine. Rafiki ya Macheda alipata jeraha kichwani wakati wa wizi.

Thursday 6 September 2012

DAVID SILVA


David Silva

David Silva
Urefu1.70 m (5 ft 7 in)
Playing positionAttacking midfielder / Winger
Club information
Current clubValencia
Namba21
Youth career
San Fernando
2003–2004Valencia
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2004–Valencia98(14)
2004–2005→ Eibar (loan)35(5)
2005–2006→ Celta Vigo (loan)34(4)
Timu ya Taifa ya Kandanda
2002–2003Spain U1720(5)
2004–2005Spain U1914(5)
2005Spain U205(4)
2004–2006Spain U219(7)
2006–Spain32(6)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only and correct as of 02 November 2009.
† Appearances (Goals).
‡ National team caps and goals correct as of 18 November 2009
David Silva
David Josué Jiménez Silva (aliyezaliwa Januari 8, 1986 Arguineguín huko Las Palmas) ni mchezaji mpira mhispania ambaye kwa sasa anachezea timu ya Valencia FC na timu ya taifa ya Uhispania.
Silva ana uwezo wa kucheza kwa upande wowote au kama namba 10 ya kiasili, na wakati mwingine kama mshambulizi msaidizi. Ni mchezaji mwenye mwili mdogo, na mara nyingi hulinganishwa na Aimar Pablo, alipochukua nafasi yake huko Valencia, akivalia nambari iliyohusishwa sana na Aimar; namba 21.

Yaliyomo

  [ficha

[hariri]Wasifu wa Klabu

Silva alianza kucheza mpira wa kulipwa msimu wa 2004-05 katika Ngazi ya pili katika timu ya SD Eibar, akiwa amekopwa kutoka Valencia CF na alicheza mechi 35 katika daraja hilimna kufunga mabao matano.Msimu uliofuatia, alikopwa tena, lakini wakati huu alikopwa na timu ya Celta de Vigo, ambapo alicheza mechi 34, na kufunga mabao manne. Baada ya kucheza mechi mbili ambazo aliingia uwanjani katika dakika za mwisho za mechi hizo, ambapo mechi ya kwanza iliisha kwa Celta de Vigo kushinda 2-0 nyumbani dhidi ya Malaga CF tarehe 28 Agosti 2005. Silva akamaalizia msimu huo kama mshambulizi bora huku timu hii ya Kigalisia ikifuzu katika kombe la UEFA moja kwa moja kutoka daraja la pili. Katika misimu miwili, alikosa kucheza mechi sita tu ilhali alifunga mabao 14 (bao la kwanza alilifunga tarehe 5 Novemba, 2006 katika tasa ya 1-1 ugenini RCD Espanyol). Baada ya kutocheza kwa muda wa miezi mitatu kutokana na jeraha la kisigino ambapo alifanyiwa upasuaji, [2] Silva alirejea kikosini katikati mwa Desemba.[1]

[hariri]Wasifu wa Timu ya Taifa

Silva aliwakilishwa Uhispania akiwa na Cesc Fabregas mara ya kwanza mwaka wa 2003 katika michezo ya ubingwa duniani ya FIFA ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 huko Finland, ambapo alifunga mabao matatu. Mwaka wa 2006, alijiunga na timu ya Uhispania ya wachezaji wasiozidi umri wa 21 na alifunga mabao manne katika kombe la vijana duniani la FIFA mwaka 2005; hii ilimwezesha kunyakua nafasi ya 4 katika orodha ya wafungaji bora, pamoja na mshambulizi mwitaliano Graziano Pellè.
Silva alichezea mara ya kwanza timu kuu ya Uhispania tarehe 15 Novemba 2006 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Romania ambapo timu yake ilishindwa 1-0 nyumbani. Aliendelea kutajwa katika orodha ya timu ya Uhispania baada ya kuchangia vizuri katika mechi zake za kwanza. Tarehe 22 Agosti 2007, Silva aliifungia Uhispania mabao yake ya kwanza kikosini mwa Uhispania, na alifunga mara mbili katika mechi hiyo ambapo waliishinda Ugiriki 3-2 katika mechi ya kirafiki. Baadaye aliitwa ajiunge na kikosi cha wachezaji 23 ambao wangeiwakilisha nchi yao katika dimba la Euro 2008.
Katika nusu fainali Silva alifunga bao la tatu la Uhispania dhidi ya Urusi baada ya ushambulizi wa haraka ambayo Cesc Fabregas alimpigia krosi Silva, ambaye alitia mpira ndani ya lango la Igor Akinfeev kwa kutumia mguu wake wa kushoto. [4]
Katika fainali, Silva alihusika katika tukio fulani na mjerumani Lukas Podolski. Baada ya kumvuta Podolski chini, Podolski alimwenedea Silva na kuzua ubishi mkali ambao haukuadhibiwa na mwamuzi. Muda mfupi baadaye, kocha wa timu ya Uhispania, Luis Aragonés, alimwondoa Silva na kuleta Santi Cazorla ili kuzuia wezekano la vita. [5]

[hariri]Mabao ya kitaifa

David Silva: International goals
GoalDateVenueOpponentScoreResultCompetition
12007-08-22Toumba Stadium, Thessaloniki, Greece Ugiriki2-22-3Friendly
22007-08-22Toumba Stadium, Thessaloniki, Greece Ugiriki2-32-3Friendly
32008-06-26Ernst Happel Stadion, Wien, Austria Urusi0-30-3UEFA Euro 2008
42009-09-5Riazor, A Coruña, Spain Ubelgiji1-05-02010 World Cup qualifying
52009-09-5Riazor, A Coruña, Spain Ubelgiji4-05-02010 World Cup qualifying
62009-10-14Bilino Polje, Zenica, Bosnia and Herzegovina Bosnia na Herzegovina0-22–52010 World Cup qualifying

[hariri]Tuzo

Valencia

[hariri]Tuzo alizopokea na Nchi

  • Dimba la Euro: 2008
  • Kombe la mashiriko ya FIFA: Nafasi ya Tatu 2009
  • Kombe le Ubingwa duniani la waliochini ya miaka 17: nafasi ya pili mwaka 2003
  • Kombe le Ubingwa duniani la waliochini ya miaka 19: nafasi ya pili mwaka 2003
  • Kombe la Ulaya la waliochini ya miaka 19: 2004

[hariri]Tuzo za Kibinafsi

Wednesday 5 September 2012

AKON


Akon

Akon
Akon.jpg
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwaAliaune Badara Akon Thiam
Amezaliwa30 Aprili 1973 (umri 39)
Asili yakeDakar, Senegal
Aina ya muzikiHip hopR&BPop
Kazi yakeMwanamuziki
Mtayarishaji
Mtunzi wa nyimbo
Miaka ya kazi1996–hadi leo
StudioUniversalSRCKonvict MuzikUpFront
Ameshirikiana naDJ KhaledLil WayneColby O'DonisKardinal Offishall,Snoop DoggT-PainYoung Jeezy
Tovutiwww.akononline.com
Aliuane Badara Akon Thiam[1] (amezaliwa tar. 30 Aprili1973[2][3]), anayefahamika zaidi kwa jina lake la kati na ambalo analitumia kwa usanii; Akon ni chotara wa Msenegali na Mwamerika ambaye ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za R & B, mtayarishaji wa rekodi, mfanyabiashara, na mhisani. Yeye alipata umashuhuri katika mwaka wa 2004 kufuatia kutolewa kwa wimbo wa "Locked Up", uliokuwa wa kwanza kutoka kwa albamu yake ya kwanza iliyoitwa, Trouble. Albamu yake ya pili, Konvicted, ilimwezesha kuteuliwa kushindania tuzo la Grammy kutokana na wimbo wa "Smack That". Yeye kufikia sasa ameanzisha kampuni mbili za kurekodi ambazo ni, Konvict Muzik na Kon Live Distribution. Yeye anajulikana kama mojawapo wa waimbaji waliofanikiwa na hodari zaidi wa mtindo wa R & B wa karne ya 21, apataye zaidi ya dola milioni 30 kwa mwaka . Haya ni kulingana na jarida la Forbes. Akon mara nyingi hushirikiana na wasanii wengine na kwa sasa ameshirikishwa katika zaidi ya nyimbo 200 na ana nyimbo 36 kwenye orodha ya Bango la nyimbo 100 mashuhuri. Yeye ni msanii wa kwanza kuchukua nafasi ya kwanza na ya pili mtawalia, kwa mara mbili, kwenye chati za Mabango ya nyimbo 100 mashuhuri. Yeye ameteuliwa mara 6 kushindania tuzo ya Grammy na amehusika katika utayarisha ji wa nyimbo za wasanii kama vile Lady GagaT-PainLeona Lewis miongoni mwa wengine. Yeye amekuwa na nyimbo 19 kwenye kitengo cha nyimbo 20 bora duniani kote.

Yaliyomo

  [ficha

[hariri]Historia

Akon amedai katika mahojiano kwamba jina lake kamili ni Aliuane Damala Bouga Time Puru Nacka Lu Lu Lu Badara Akon Thiam [4]ingawa kuna utata na mjadala kuhusu jina lake halisi na tarehe yake ya kuzaliwa. Akon kwa kawaida anajulikana kama Aliuane Thiam. Juu ya jina lake refu , jina kamili la Akon limeripotiwa kuwa Aliaune Badara Thiam na Alioune Badara Thiam na mtandao wa About.com unadai kwamba jina lake la katikati halijawahi kuthibitishwa. Kuhusu tarehe yake ya kuzaliwa, baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kwamba Akon alizaliwa mwaka 1981. Taasisi zingine, ikiwemo AP, wanadai kuwa Akon alizaliwa mwaka wa 1973, na mamake alisaidiwa kujifungua na daktari msenegali aitwaye Magueye Seck.
Hati za kisheria zilizotolewa na The Smoking Gun zinaonyesha jina la Akon kama Aliuane Damala Thiam na tarehe yake ya kuzaliwa kama 1973/04/30 [5] au 1973/04/16,[6] hata hivyo shirika la BBC linasema kuwa Akon alizaliwa tarehe 14 Oktoba, 1981.

[hariri]Maisha Yake ya Utotoni

Akiwa mwanawe mcheza ala za muziki aliyesifika kutoka Senegali aliyejulikana kama Mor Thiam, Akon alikulia katika mandhari ya muziki na alifundishwa kucheza ala kadhaa ikiwemo djembe. Yeye alizaliwa St Louis, Missouri, USA ili kukwepa shughuli za kutafuta kibali cha uhamiaji, lakini aliishi mjini Dakar, Senegal hadi alipofikisha umri wa miaka 7, kisha akabadilishana kati ya kuishi Senegali na Marekani hadi alipofikisha umri wa miaka 15, alipohamia kabisa mjini Jersey, New Jersey.
Wakati Akon aliposemaka kuwa katika jela kwa miaka 3, alianza kutambua kipawa chake cha muziki na akaanza kujivunia historia ya muziki iliyokuwa kwenye familia yake. Mchanganyiko wake wa kipekee wa mtindo wa Afrika Magharibi, ujuzi wake na hatimaye mitindo yake ya densi iliwavutia wakuu wa shirika la Universal. Akon alianza kuandika na kurekodi nyimbo katika studio yake ya nyumbani. Tepu zake zilifika kwenye kampuni hiyo ya SRC/Universal, ambayo ilitoa albumu (LP) yake ya kwanza, Trouble, mnamo juni 2004. Albamu hii ni mseto wa mtindo mwororo wa Akon wa Afrika Magharibi Ukichanganywa na MIDU kutoka Pwani ya Mashariki na Kusini. Nyimbo nyingi za Akon huanza kwa sauti ya kufunguka kwa mlango wa jela naye akitamka neno "Konvict".

[hariri]Maisha yake ya kibinafsi na madai

Akon ni Muislamu, na anasema kwamba hajawahi kulewa pombe kutokana na imani yake. Kumekuwa na madai kuwa ana wake watatu, hata hivyo amebaini kuwa ana mmoja tu, aitwaye Tomeka. Akon alidai kuwa amepata watoto sita na wanawake watatu tofauti katika mahojiano na jarida la Blender. Akon pia anadai kuwa na uhusiano mzuri sana na watoto wake wote, na kwamba yeye anataka kukinga familia yake kutokana na jicho la umma. Yeye pia anasema kwamba dini yake ilimfanya kuwa mtu bora, na inampa mwongozo wa jinsi ya kutagusana na watu wengine maishani.
Yeye pia ana shirika lake la kutoa msaada kwa watoto wasiojiweza barani Afrika liitwalo Konfidence Foundation. Akon anamiliki mgodi wa almasi katika Afrika ya Kusini na anakanusha uwepo wa almasi za damu (zinajulikana pia kama " almasi za vita") akisema, "Hata siamini kuwa kuna almasi za vita. Hiyo ni filamu tu. Hebu fikiria. Hakuna mtu yeyote aliyewahi kufikiria chochote kuhusu almasi ya vita hadi wakati filamu hii ilipotolewa. Hata hivyo,tangu wakati huo yeye amesema kuwa hakubali kwamba almasi za damu zipo, na kwamba anamiliki nusu ya mgodi mmoja uliopo Afrika ambao unatia jitihada kuepuka matumizi ya almasi za damu huku wakizifaidi jamii zinazowazunguka. Inadaiwa kuwa aliwahi kushiriki katika ulanguzi wa madawa ya kulevya, lakini yeye amekanusha akisema hajawahi kutumia madawa haya, ingawa maneno ya baadhi ya nyimbo zake yanakinzana na makanusho yake.
Jarida la "The Smoking Gun" liliripoti, mnamo Aprili 2008, kwamba historia ya Akon ya kufungwa jela imeongezwa chumvi. Madai ya kuwa Akon alikuwa sehemu ya genge la wizi na kwamba alikaa miaka mitatu gerezani yalikabiliwa na rekodi za mahakama na za mahojiano na wachunguzi waliohusika katika kesi yake.
Kulingana na makala ya jarida la "Smoking Gun" , Akon hakushtakiwa na hatia yoyote ya uhalifu na hakutumikia kifungo chochote gerezani kati ya 1999-2002 kama alivyodai hapo awali. Yeye alisema kwamba jaribio la jarida la "The Smoking Gun" la kumharibia jina halina maana yoyote kwani hilo ni jambo analojaribu kulisahau." Akon alisema kuwa yeye hajawahi kukaa kwenye jela kipindi cha miaka 3 mfululizo, lakini amewahi kukaa vipindi vifupu vifupi ambavyo vimefikia miaka mitatu, na anasema kwamba huko ni kutoelewa kwa makala ya Smoking Gun. Japo ana historia ya uhalifu , Akon anatangaza kwamba amebadilisha mienendo ya maisha yake.

[hariri]Kazi

[hariri]2004-05: Albamu ya kwanza: Trouble

Albamu yake ya kwanza, 'Trouble' ilitolewa Juni tarehe 29, 2004. Albamu hii ina nyimbo kama "Locked Up" na "Lonely", "Belly Dancer (Bananza)", "Pot of Gold", na "Ghetto." Albamu hii ndiyo iliyokuwa ya kwanza kutolewa na kampuni yake mpya ya kurekodi ya Konvict Music. Msukumo wa kuimba wimbo wake wa kwanza ulitokana na miaka mitatu aliyokaa kwenye jela kwa sababu ya 'kuiba'. Wimbo wa "Locked Up" uliorodheshwa kwa nyimbo 10 bora nchini Marekani na tano bora nchini Uingereza. "Wimbo wa "Ghetto" ulivuma kwenye redio wakati ulipochanaganywa upya na DJ Green Lantern na kujumuisha mistari kutoka wasanii 2Pac na The Notorious B.I.G.
Katika mwaka wa 2005, yeye alitoa wimbo "Lonely" (ambao ni sampuli ya wimbo wa Bobby Vinton wa "Mr Lonely"). Wimbo huo uliorodheshwa miongoni mwa nyimbo tano bora kwenye orodha ya Bango laynyimbo 100 mashuhuri, na ukaongoza kwenye chati katika nchi ya Australia, Uingereza na Ujerumani. Albamu yake pia ilifikia namba moja nchini Uingereza katika mwezi wa Aprili, 2005. Wakati runinga ya muziki ya 'The Box' ilikuwa ikichagua nyimbo kumi bora za wiki , uchaguzi ambao ulikadiriwa kwa kiasi cha mara ambayo video hiyo iliombwa na mashabiki, wimbo wa Akon "Lonely" ndio ulioongoza kwenye chati hiyo kwa muda mrefu zaidi, kwani ulikaa wiki kumi na tano. Akon kisha alitoa wimbo, akishirikiana na msanii kutoka New Zealand aliyeitwa Savage, ulioitwa 'Moonshine', na ambao ulivuma huko New Zealand na Australia, na ukawa namba moja katika chati ya New Zealand. Katika mwaka wa 2005, alishiriki katika albamu ya kwanza ya mwimbaji Young Jeezy katika wimbo wa "Soul Survivor." Mwezi Desemba mwaka uo huo meneja wake, Robert Montanez aliuawa kwa kupigwa risasi baada ya mzozo huko New Jersey.

[hariri]2006-07: albamu ya Konvicted


Akon performing with Gwen Stefani on The Sweet Escape Tour.
Albamu ya pili ya Akon, Konvicted ilitolewa tarehe 14 Novemba, 2006. Ilikuwa na nyimbo alizoshirikisha waimbaji kama EminemSnoop Dogg na Styles P. Wimbo wa kwanza "Smack That" aliomshirikisha Eminem ulitolewa Agosti 2006 na ukashika nafasi ya pili kwenye orodha ya Bango la nyimbo 100 mashuhuri kwa wiki tano mfululizo. Wimbo wa "I Wanna Love You,"(akimshirikisha Snoop Dogg) ndio uliokuwa wimbo wa pili uliotolewa Septemba, na ukawa ndio ambao ungekuwa wa kwanza wa Akon kuwa namba moja kwenye orodha ya Bango la nyimbo 100 mashuhuri, na wa pili wa Snoop. Wimbo huu wa "I Wanna Love You" uliongoza kwenye chati za Marekani kwa muda wa wiki mbili mfululizo. Katika Januari 2007, wimbo wa tatu "Don't Matter" ambao ulikuwa wimbo wa kwanza, alioimba bila kumshirikisha yeyote, kuwa namba moja, na wimbo wake wa pili kuichukua nafasi hiyo kwenye chati ya nyimbo 100 mashuhuri, ulitolewa. Wimbo wa "Mama Afrika" ulitolewa kama wimbo wa Ulaya mwezi Julai 2007, na kufikisha jumla ya nyimbo nne zilizokuwa zimetolewa kutokwa kwenye albamu hiyo iliyokuwa imefika namba 47 nchini Uingereza.
Kutolewa ya toleo la 'Platinum (Deluxe)' la albamu hii kulifanyika wakati mmoja na kutolewa kwa "Sorry, Blame It on Me", uliokuwa wimbo wa tano kutoka kwa albamu hiyo, na ulioshika nafasi ya saba kwenye orodha ya nyimbo 100 mashuhuri katika mwezi Agosti 2007. Toleo hilo la Deluxe lilitolewa kikamilifu tarehe 28 Agosti, 2007. Wimbo wa mwisho katika albamu hiyo ulithibitishwa na Akon kuwa "Never Took the Time." [7] Albamu ya Konvicted ilipata kushika nafasi pili kwenye orodha ya Bango la nyimbo 200 mashuhuri,na kuuza nakala 286,000 katika wiki yake ya kwanza. Baada ya wiki sita tu, albamu ya Konvicted iliuza zaidi ya nakala milioni moja nchini Marekani na zaidi ya nakala milioni 1.3 duniani kote. Albamu hii ilithibitishwa kuhitimu kiwango cha platinumu baada ya wiki saba, na baada ya wiki kumi na sita ilithibitishwa kuhitimu kiwango hiki, cha platinamu, kwa mara mbili. Albamu hii ilikaa katika orodha ya nyimbo ishirini za kwanza kwenye orodha ya ' Bango/0} la nyimbo 200 mashuhuri kwa wiki 28 mfululizo na ilipata kushika nafasi ya pili katika nyakati nne tofauti. Mnamo November 20, 2007, shirika la RIAA ilithibitisha albamu hii kuwa imehitimu kiwango cha 'triple platinum' na rekodi milioni 3 zikiwa zimeuzwa Marekani. Imeuza zaidi ya nakala milioni 4 duniani.
Mnamo Oktoba 5, 2006, Akon alivunja rekodi ya orodha ya nyimbo 100 mashuhuri, kwani wimbo wake wa "Smack That" ulipata mafanikio ya juu zaidi kwa kuruka kutoka namba 95 hadi namba 7. Kupanda huko kulitokana na wimbo huo kushika nafasi ya sita kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya Hot Digital Songs kutokana na mipakuo 67000. Rekodi hiyo imevunjwa mara kadhaa tangu wakati huo. Mnamo Desemba 2006, wimbo wa Akon wa "Smack That" ulikuwa umependekezwa kushindana katika kategoria ya Best Rap / Sung Collaboration katika mashindano ya 49 ya Grammy Awards, lakini ulishindwa na ule wa Justin Timberlake na wa T.I. wa "My Love".

[hariri]Miradi aliyoshirikiana na wasanii wengine

  • Mwaka wa 2006, Akon alianza kampuni yake mpya ya Kon Live Distribution chini ya Interscope Records. Msanii wake wa kwanza kusaini mkataba naye alikuwa ni Ray Lavender.
  • Yeye alishirikishwa kwenye albamu ya hivi karibuni ya Gwen StefaniThe Sweet Escape. Yeye alishiriki katika wimbo wa anwani ya jalada na wimbo wa pili, "The Sweet Escape." Akon alitayarisha wimbo huo. Mnamo Desemba 10, 2006, Akon na Stefani walihudhuria 'Saturday Night Live' kama wageni wanamuziki, hata hivyo hawakuimba wimbo huo kwa sababu Stefani alikuwa bado hajajifunza maneno yake. Hata hivyo, Akon aliimba wimbo huo mbele ya hadhira, katika hafla ya American Idol tarehe 28 Machi 2007 kutokana na Gwen Stefani kushiriki kama kocha usiku uliotangulia. Wimbo huu wa "The Sweet Escape" umefikia # 2 kwenyeBango la nyimbo 100 mashuhuri.
  • Akon alishirikiana na Chamillionaire kwenye tepu yake ya, Mixtape Messiah 2, akishiriki kwenye kibao "Ridin 'Overseas" ambacho alikuwa amekitayarisha. Tepu hii ilikuwa tayari kupakuliwa kutoka tovuti ya Chamillionaire kuanzia Desemba 24, 2006.
  • Katika mwaka 2006, baada ya wimbo wao wa mwaka wa 2005 uliotayarishwa na Akon, "Soul Survivor," wawili hawa walisema kuwa kuna mengi zaidi ya kutarajia kutoka kwao katika siku zijazo. Wao walitangaza kuwa kuna mipango ya kushirikiana na kutoa albamu.[8][9]
  • Akon pia alishiriki katika albamu ya Bone Thugs-n-Harmony ya Strength and Loyalty na kwenye albamu ya nane ya Three 6 Mafia,Last 2 Walk, We The Best iliyotayarishwa na DJ Khaled. Aidha yeye alishiriki kwenye albamu ya Fabolous ya, From Nothin' to Somethin ', na wakashiriki wakiwa na 50 Cent katika baadhi nyimbo za Curtis. Isitoshe, yeye alishiriki kwenye [10] albamu ya 5 yaT.I , T.I dhidi ya T.I.P., [11] albamu ya tatu ya Mario Go!, [12] na wakatayarisha wakiwa na Daddy Yankee katika wimbo unaoitwa "Bring It on" kwenye albamu ambayo ilitolewa tarehe 5 Juni, 2007.[13]
  • Tarehe 7 Julai, 2007 Akon alitumbuiza watu katika hafla ya American leg of Live Earth.
  • Mnamo Novemba 2007, Akon alirekodi toleo jipya la wimbo "Wanna Be Startin 'Somethin'" wakiwa na Michael Jackson. Mwezi wa February 2008, toleo jipya la wimbo huo lilitolewa wakati wa maadhimisho ya 25 ya kutolewa upya kwa video ya Michael Jackson ya Thriller. Akon alitayatayarisha kibao cha "Echo" kilicho kwenye albamu mpya ya bendi ya wavulana ya Kilatini, Menudo, kilichotolewa katika majira ya spring ya 2008.
  • Kampuni ya 'Konvict Music' ndiyo ingehusika katika kutolewa upya kwa albamu ya kwanza ya Kat DeLuna9 Lives (albamu)ambayo ingeshirikisha Akon katika wimbo wa "Am I Dreaming."
  • Yeye pia alikuwa katika wimbo uliohusisha Aventura, Akon na Wisin Y Yandel ulioitwa "All up 2 you".
  • Katika mwezi wa Julai 2008, wimbo unaoitwa "Hold My Hand" ulisambaa kwenye mtandao. Wimbo huo ni wa R & B ulioimbwa kwa ushirikiano kati ya Michael Jackson na Akon, na uliotungwa na Claude Kelly. Pia kuna toleo lingine la wimbo huo linalomshirikisha Akon pekee. Pia hakuna kutajwa rasmi kwa kurekodiwa kwa wimbo huo katika aidha ya tovuti za wasanii hawa wawili ingawa Akon ameuzungumzia katika tovuti zingine tofauti. Wimbo huu haukujumuishwa katika orodha ya nyimbo za Freedom kama Akon alivyokuwa ameeleza hapo awali. Katika mahojiano na Smiley Tavis, Akon alisema kuwa Jackson alikuwa amepanga kufanya toleo moja la hali ya juu ambalo lingehusisha video ya wimbo huo lakini wimbo huo ulifichuka kwa umma. Huu ndio wimbo wa mwisho unaojulikana wa Jackson kabla ya kifo chake kilichotokea tarehe 25 Juni, 2009. Mwishoni mwa Julai ya mwaka huo, wimbo wa heshima ulioandaliwa na Akon unaojulikana kama "Cry Out Of Joy" ilifichuliwa kwenye mtandao.
  • Akon ndiye aliyekuwa pia mtaarishaji mkuu wa albamu ya nne ya Kardinal Offishall, Not 4 Sale, iliyotolewa Septemba 9, 2008. Wimbo wa mauzo wa albamu hiyo, "Graveyard Shift" ulishirikisha Akon, ukiwa pamoja na wimbo wa kwanza, "Dangerous", ambao ulipata kushika nafasi ya # 5 kwenye Bango la nyimbo 100 mashuhuri, na ulioshinda tuzo la Wimbo wa Mwaka katika mashindano ya Juno Awards ya 2009.
  • Akon alishiriki katika kuandika na kutayarisha wimbo wa "Put It on My Tab" na New Kids on the Block uliokuwa wa albamu yao ya 2008 Reunion ya The Block.
  • Akon alishiriki katika kuandika na kutayarisha wimbo wa Leona Lewis wa Forgive Me, ulio kwenye albamu yake, Spirit.
  • Kwa sasa yeye anafanya kazi na mshindi wa X Factor 2008, Alexandra Burke kwenye albamu yake ya kwanza.
  • Akon alishiriki katika kutayarisha albamu ya kwanza ya msanii wa Konvict MuzikLady Gaga iliyoitwa The Fame na akashiriki katika kuandika & kutayarisha wimbo uliovuma duniani kote wa "Just Dance", ambao pia ulishirikisha Colby O'Donis na uliopendekezwa kushindana katika mashindano ya Grammy Awards ya 51. Wimbo huu uliwapatia vijana hawa wawili wa Konvict Muzik nafasi zao za kwanza za kushindana kwenye mashindano ya Grammy na umefikia namba # 1 katika nchi zaidi ya 14, zikiwa ni pamoja na Australia, Uingereza & Marekani
  • Albamu mpya ya Flo Rida ya R.O.O.T.S. ilishirikisha Akon kwenye wimbo wa "Available".
  • Akon amerekodi wimbo na E-40 unaoitwa "Wake It Up" ulio katika albamu ya E-40 ya The Ball Street Journal. Akon anafanya majaribio na athari za 'auto-tune' katika wimbo huo.
  • Mwimbaji wa Rap, Nelly, alithibitisha kuwa Akon, Pharrell, na T-Pain walizungumza kuhusu kuunda kikundi cha kuimba muziki wa rap katika mwaka wa 2009.[14]
  • Akon pamoja na kampuni yake ya Konvict Muzik pia wanahusika katika kutayarisha albamu ya 2009 ya kikundi cha hip hop / rock,Flipsyde, inayoitwa State of Survival, itakayotolewa kupitia Kon Live Distribution na Cherrytree Records. [15]
  • Akon alifanyakazi na Whitney Houston katika kutayarisha albamu yake mpya ya mwaka wa 2009 iitwayo I Look To You. Yeye alishiriki katika wimbo wa "Like I Never Left".[16]
  • Akon alifanya kazi na kikundi cha bachata kiitwacho Aventura, na waimbaji wa ReggaetonWisin y Yandel, katika kutayarisha wimbo wao wa pili wa All Up 2 You kutoka kwa albamu ya Aventura ya The Lastthat iliyotolewa Juni.
  • Akon hivi majuzi alitia saini mkataba na Jayko, msanii wa R & B na Reggaeton kutoka Uhispania, kwenye studio yake na sasa hivi anashirikiana naye kutayarisha albamu yake inayoitwa "Marcando Territorio"
  • Albamu ya Sexy Bitch ilitolewa Julai 2009, kwa ushirikiano na DJ wa Kifaransa, David Guetta.
  • Mnamo Agosti 2009, Akon alitolewa toleo jipya la 'Beautiful' akimshirikisha BOA, mwimbaji maarufu kutoka Korea. Hata hivyo, toleo hili lilikuwa limelenga soko la Ujapani.
  • Akon pia aliimba katika wimbo akishirikiana na Colby O'Donis unaoitwa "What You Got".

[hariri]Matatizo ya kisheria

Mwezi Aprili 2007, Akon alikosolewa baada ya kucheza ngoma ya kusisimua na Danah (Deena) Alleyne, binti wa mhubiri aliyekuwa na umri wa miaka 15 wakati huo, katika klabu moja huko Trinidad na Tobago, kama sehemu ya shindano bandia, licha ya klabu hiyo kudai kuwa hawaruhusu watu walio na umri wa chini ya miaka 21, kuingia huko.[17][18] Tukio hilo lilirekodiwa na wafanyakazi wa Akon na baadaye rekodi hiyo ikapakiwa kwenye mtandao. Tarehe 20 Aprili 2007 vyombo vya habari vya mtaa, chaneli TV6, walionyesha video hiyo hadharani. Katikati ukosoaji kwenye redio, televisheni, na kutoka kwa Blogu, Verizon Wireless waliondoa nyimbo za mlio wa simu (ringitoni) zilizoshirikisha nyimbo za Akon. Verizon pia waliamua kutogharamia ziara ya The Sweet EscapeTour ambapo Akon alitarajiwa kuimba mwanzoni mwa onyesho kabla ya Gwen Stefani. kuingia jukwaani [19] Hata hivyo, kampuni ya Universal Music Grouphaikuchukua hatua dhidi ya Akon, bali iliamrisha tu video hiyo iondolewe kutoka kwa tovuti ya YouTube kutokana na ukiukaji wa hakimiliki. Mtoa maoni na mwanzilishi wa Parents Television councilBrent Bozell aliita hatua hii "ukosefu wa uwajibikaji wa pamoja."[20]
Wachambuzi wa kisiasa Michelle MalkinLaura Ingraham, na Bill O'Reilly walimkosoa Akon kwa "kushusha hadhi ya wanawake."[21][22] Malkin alipakia ufafanuzi kuhusu Akon kwenye tovuti ya YouTube, kwa kutumia vijisehemu kutoka kwa video za muziki pamoja na onyesho la Trinidad, na kampuni ya Universal Music Group ikalazimisha kuondolewa kwa video kwa kuwapatia ilani ya kuondoa yaDMCA.[23] Wakfu wa The Electronic Frontier Foundation ilimuunga mkono Malkin katika kupinga kuondolewa huko kwa kusema kuwa hayo ni matumizi mabaya ya hakimiliki, akirejelea matumizi ya haki. [24] Mwezi Mei 2007, UMG walibatiliza madai yao ya video hiyo, na ikarejeshwa kwenye tovuti ya YouTube.
Tarehe 3 Juni 2007, kwenye onyesho la WSPK 's KFEST katika Uwanja wa Dutchess huko Fishkill, New York, mhudhuria mmoja wa onyesho hilo alimtupia Akon kifaa fulani alipokuwa jukwaani. Akon aliuliza umati kumtambua aliyekuwa ametupa kitu hicho na wampeleke jukwaani. Walinda usalama walimshika kijana huyo na kumpeleka hadi jukwaani. Akon kisha alimvuta kutoka kwa umati na kumbeba kwa mabega yake. Kisha akamtupa kijana huyo kwenye umati. Video ya tukio hilo ilitazamwa tena na polisi wa Fishkill.[25]Akon amedai kuwa tukio hilo lilikuwa la maigizo na kwamba yeye alilitumia kuanzisha rekodi yake iliyofuata.[26] Mashtaka ya kuhatarisha ustawi wa kijana, kumdharau, na kumdhulumu, ukiukaji, yaliandikwa, kulingana na ofisa wa polisi Donald F. Williams, na Akon alipelekwa kortini ili kujibu mashtaka haya mawili tarehe 3 Desemba, 2007 katika korti la mji wa Fishkill.[27]

[hariri]2008-hadi leo: Albamu ya Freedom

Akon alitoa albamu yake mpya Freedom mnamo Desemba 2, ambayo imetoa nyimbo nne: "Right Now (Na Na Na)", "I'm So Paid"(akishirikiana na Lil Wayne na Young Jeezy), "Beautiful" (akimshirikisha Kardinal Offishall na Colby O'Donis) na "We Don't Care",Wimbo wa 'We Don't Care' umeshindwa kupanda juu kwenye chati za nchi nyingi, na kufika tu namba 61 katika UK na namba 91 katika Australia kufikia sasa. Albamu hii imefikia kiwango cha dhahabu kwa kuuza zaidi ya nakala 600,000.[onesha uthibitisho]. Baada ya kifo cha ghafla cha mfalme wa Pop Michael Jackson, ambaye Akon alikuwa akifanya kazi naye katika miaka ya mwisho ya Jackson Akon alitoa wimbo wa kuonyesha heshima unaoitwa "Cry Out Of Joy". Akon & Michael Jackson walikuwa marafiki wa karibu katika wakati huu wa mwisho wa maisha ya Jackon.
Akizungumza kuhusu uhusiano wake na Michael Jackson kwa mwandishi anayesifika wa UK wa R & B, Pete Lewis, aliyeshinda tuzo kwa wimbo 'Blues & Soul' katika Oktoba 2008, Akon alisema: "Mike ni Mfalme wa Pop, na nadhani kuwa ni kutimia kwa ndoto kwa msanii yeyote mkuu / mtunzi / mtayarishaji kuweza kufanya kazi na wale waliobora katika biashara! Unajua, kufanya kazi na mtu kama Mike - ambaye amebuni fursa, akafungua milango kwa watu wengi, na kupata mafanikio makubwa katika ulimwengu wa muziki, basi - ni tajriba ambayo imetosha kuipokea kwa mtu ye yote! Yaani, wakati mimi nilisafiri kwa ndege hadi Vegas ili nikutane naye, ilikuwa ni kama tulikuwa tumejuana kwa MIAKA! UKWELI! 'Kwa sababu kimuziki tulikuwa na maoni sawa! Uhusiano wetu ulikuwa wa ajabu! Na, kwa hulka zake, alikuwa ndiye mtu mzuri na mnyenyekevu zaidi niliyewahi kukutana naye milele! Yaani, sisi hata tulienda kutazama filamu pamoja - katika wakati wa mchana! Ambayo ilikuwa ni tajriba spesheli! [28]
David Guetta alishirikiana na Akon katika Sexy Bitch, wimbo wa kwanza wa Akon, na umevuma duniani kote. Wimbo huu ambao umekuwa namba # 1 katika zaidi ya nchi 5, na kushika nafasi ya 12 kwenye chati ya Biango la nyimbo 100 mashuhuri, umeshirikishwa kwenye albamu ya Guetta ya One Love. Na ni wimbo wake wa 19 kuingia kwenye orodha ya nyimbo bora 20 duniani kote.
Albamu ya nne ya Akon, Stadium Music inatarajiwa kutolewa 2010.[29]

[hariri]Televisheni na filamu

Akon amethibitisha kwamba anafanyia kazi mradi wa kuanzisha kipindi maalum kwenye televisheni. Kipindi hicho kitaitwa "My Brother's Keeper" na kitahusisha ndungu wawili wa Akon wanaokaribia kuwa mapacha na ambao watazunguka Atlanta wakijifanya kuwa wao ni yeye wa kuwapumbaza watu. Watajaribu kupata huduma za VIP, wasichana na vitu vya bure. Akon amedai kwamba mara nyingi watu huko Atlanta wamedhani kuwa ndugu zake ni yeye na huu ndio msingi wa kipindi hiki.[26]
Akon ana mipango ya kurekodi filamu nzima yenye jina Illegal Alien. Filamu hii imejikita katika baadhi ya matukio ya maisha yake na mwigizaji Mekhi Phifer atamwigiza yeye. Mbali na hayo, Akon alithibitisha katika mahojiano na tovuti ya Poland ya INTERIA.PL mnamo Agosti 2007, kwamba yeye anarekodi filamu inayoitwa "Cocain Cowboys", ambayo inazungumzia maisha ya Jon Roberts, mkuu wa kateli ya Medellin (walanguzi wa madawa ya kulevya wa Colombia).[30] Yeye pia alishirikishwa kwenye tangazo la kibiashara na la kuimba la Verizon Wireless Snitch wakiwa na Obie Trice katika tukio lililoitwa CSI: Crime Scene Investigation "Poppin' Tags."
Mnamo November 30, 2007, Akon aliingia kwenye nyumba ya Big Brother katika Pinoy Big Brother Celebrity Edition 2 kama mgeni ili washiriki waweza kukutana naye kwa sekunde 100 tu.
Yeye pia alionekana kwenye toleo la tarehe 17 Novemba 2008 la WWE Raw, huku Santino Marella akimtaja katika hotuba yake. Kwa sababu ya athari za Kiitaliano za Santino, yeye alilitamka jina la Akon vibaya, yaani "Akorn".
Mnamo April 27, 2008, Akon alionekana na Colby O'Donis katika Dance on Sunset.

[hariri]Mtindo

Mnamo Februari 2007, Akon alianzisha aina yake ya mavazi, Konvict Clothing. Mavazi haya yalishirikisha mavazi yanayovaliwa mitaani kama jeans za kitambaa cha denimu, fulana zilizo na kofia, t-shati na kofia. Aliuane ni toleo la juu, ambalo linalenga wanaume na wanawake, na linalojumuisha makoti ya aina ya bleza, jeans za kitambaa cha denimu na vitu vingine. Timothy Hodge alionekana kwenye kipindi cha MTV cha Direct Effect wakiwa na Akon wakiwa wanajaribu kukuza mauzo ya mavazi ya Konvict line.[31]

[hariri]Diskografia

Makala kuu ya: Akon discography

[hariri]Tuzo na Uteuzi

Akon awards and nominations
[ficha]Awards and nominations
AwardWinsNominations
American Music Awards
13
Grammy Awards
05
MTV Video Music Awards
04
Totals
Awards won1
Nominations12
Akon alipokea uteuzi mara nne ya kushindana kwenye mashindano ya Grammy ya 2008. Uteuzi huo ulikuwa ni katika kategoria za Best Pop Collaboration with Vocals kwa wimbo"The Sweet Escape" wakishirikiana na Gwen Stefani, Best R & B Performance na waimbaji wawili ama kikundi kwa wimbo "Bartender" wakishirikiana na T-Pain, Best Contemporary R & B Album kwa Konvicted, na Best Rap / Sung Collaboration na "I Wanna Love You" wakishirikiana na Snoop Dogg. Tuzo tu ambalo Akon amepokea ni laMwimbaji wa Kiume wa Soul / R & B anayependwa zaidi kutoka mashindano yaAmerican Music Awards ya mwaka wa 2007. Ujumla, Akon amepokea tuzo moja kutokana na uteuzi wa mara kumi na mbili.

[hariri]Shindano la American Music Awards

Shindani la American Music Awards ni hafla ya kila mwaka iliyobuniwa na Dick Clarkkatika mwaka wa 1973. Akon amepokea tuzo moja kutokana na uteuzi mara tatu.[32][33]
YearNominated workAwardResult--2007 | | rowspan = "3" | Akon | |Favourite Soul / R & B Male Artist | | style="background: #99FF99; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="yes table-yes2"|Won--| style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated--Msanii wa Kiume wa Pop / Rock anayependwa | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated

[hariri]Shindano la Grammy Awards

Tuzo za Grammy Awards hutolewa kila mwaka na National Academy of Recording Arts and Science la Marekani. Akon ameteuliwa kwa mashindano mara matano.[32][34]
YearNominated workAwardResult--2007 | | "Smack That" (na Eminem) | |Best Rap / Sung Collaboration | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated--2008 | | "The Sweet Escape"(with Gwen Stefani) | | Best Pop Collaboration with Vocals | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated--"Bartender" (with T-Pain) | | Best R & B Performance by a Duo or Group | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated--Konvicted | | Best Contemporary R & B Album | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated--"I Wanna Love You" (na Snoop Dogg) | | Best Rap / Sung Collaboration | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated

[hariri]Tuzo za MTV Video Music Awards

Tuzo za MTV Video Music Awards ni hafla ya mwaka iliyoanzishwa mwaka 1984 na MTV. Akon ameteuliwa kwa mashindano mara nne.[32][35][36]
YearNominated workAwardResult--2005 | | "Locked Up" | | MTV2 Award| | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated--2007 | | Akon | |Male Artist of the Year | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated--Most Earthshattering Collaboration | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated--| Most Earthshattering Collaboration | | style="background: #FDD; color: black; vertical-align: middle; text-align: center; " class="no table-no2"|Nominated

[hariri]Ziara