Yerusalemu
Yerusalemu | |||
Ukuta wa Maombolezo na Kuba ya Mwamba mjini Yerusalemu | |||
| |||
Jina laKiebrania | יְרוּשָׁלַיִם (Yerushalayim) | ||
Jina laKiarabu | القـُدْس (al-quds); rasmi: أورشليم القدس (urshalim-al-quds) | ||
Maana ya Jina | Kiebrania: "Urithi wa amani", Kiarabu: "(Mji) mtakatifu" | ||
Utawala | Mji | ||
Wilaya | |||
Wakazi | 724,000 (Wayahudi 68%, Waislamu 30%, Wakristo 2%) (2006) | ||
Eneo | 126,000 (126 km²) | ||
Meya | Nir Barkat | ||
Tovuti rasmi | www.jerusalem.muni.il |
Yerusalemu (mara kwa mara pia Kudisi) (kwa Kiebrania ירושלים Yerushalayim, kwa Kiarabu: القدس al-Quds) ni mji wa Mashariki ya Kati wenye pande mbili. Kwa upande mmoja ni mji mkuu wa Israel. Kwa upande mwingine Yerusalemu ya mashariki inatazamiwa kuwa mji mkuu wa Palestina ingawa imetawaliwa na Israel pia tangu 1967. Israel imetangaza tangu 1980 Yerusalemu yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi za dunia hazikubali azimio hili hivyo balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Yerusalemu.
Yerusalemu ina historia ndefu sana. Ni mji muhimu katika dini tatu zinazofuata imani ya Abrahamu, yaani Uyahudi, Ukristo na Uislamu.
- Ukuta wa Maombolezo ni patakatifu pa Wayahudi wanaokwenda kuhiji na kuomboleza kwenye hayo mabaki pekee ya Hekalu ya Yerusalemu: ni ukuta uliojengwa na Mfalme Solomoni ili kuzuia vifusi vilivyojaza bonde la mji wa Mfalme Daudi kadiri ya Biblia.
- Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu kama mahali pa ufufuko wa Yesu Kristo ni patakatifu pa Wakristo muhimu kuliko mahali pengine pengi panapotajwa katika Agano Jipya au kuheshimiwa kulingana na matukio ya neema katika historia ya Kanisa.
- Msikiti wa Al-Aqsa pamoja na msikiti wa Kuba ya Mwamba ni mahali patakatifu pa Waislamu palipotajwa katika Korani; Waislamu huamini ya kwamba hapa ni mahali pa miraji ya Mtume Muhammad.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Yerusalemu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |