member

Sunday 12 January 2014

Professor Jay

Wednesday 1 January 2014

Bill Gates

Bill Gates

Bill Gates (2007)
Bill Gates - (William Henry Gates III) Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, mtu tajiri sana duniani na mwanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali.
Bill Gates ni mwanzilishi, mwenyekiti na mbinifu mkuu wa programu za kampuni ya ya Microsoft, kampuni ya programu yenye mafanikio zaidi duniani, inayoaminika kwa utengenezaji wa programu zilizo na nguvu na ubunifu hali zikiwa bado zenye utumizi mwepesi. Microsoft sasa inaajiri zaidi ya watu elfu hamsini na tano katika nchi themanini na tano.
William Gates III H anajulikana kama Bill Gates alizaliwa tarehe 28 Oktoba 1955 na kulelewa katika kijiji cha Seattle pamoja na dada zake wawili. Katika umri wake mdogo Bill Gates alivutiwa na utengenezaji wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini Seattle. Akiwa huko shuleni Seattle, Bill Gates alikutana na Paul Allen, mwanafunzi mwenzake wakawa marafiki. Hapo ndipo wakaanza kutumia tarakilishi ndogo ya shule kujiendeleza ujuzi wao.
Waliajiunga na kampuni ya kompyuta, malipo yao ikiwa ni kutumia tarakilishi yenye nguvu zaidi. Kazi yao ilikuwa ni kutafuta nukshi katika mitambo ya kompyuta, wakati huohuo waliweza kijifunza lugha mpya za kompyuta. Bill akaenda kwenye Chuo Kikuu cha Harvard. Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paulo kuandika toleo jipya la programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair 8800.Kampuni hiyo iliridhishwa na kazi ambayo Bill Gates na Paul Allen waliofanya na programu hiyo ikapewa leseni. Jambo hili liliwachangia Gates na Allen Kuanzisha kampuni ya Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea kampuni zingine programu. Bill Gates aliacha masomo yake katika chuo kikuu cha Harvard na kujishughulisha muda wake wote katika biashara.
Mapumziko yao yalikuja walipotengeneza mfumo wa kuendesha kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika katika kompyuta ya kwanza ya kibinafsi ya IBM. Baadaye waliweza kuzishawishi kampuni zingine zinazotengeneza kompyuta kutumia mfumo huo wa MS-DOS. Mfumo huu mpya wa MS-DOS ulipata umaarufu katika soko miaka ya 1980 na baadaye, Microsoft pia ilianza kutengeneza programu kama vile neno sindikizi.
Microsoft ilitangaza mfumo mpya wa uendeshaji wa kompyuta uitwao Windows 1.0 mwaka wa 1983, ambao ulikuwa na grafiksi bora na pia uliwezesha kufanya zaidi ya jambo moja kwa wakati mmoja. Hata hivyo hakuwa bidhaa nyingine iliyotolewa miaka mbili baadaye hadi mwaka wa 1985, kwa kuwa ni programu chache zilizoweza kuendeshwa katika mfumo huu wa Windows 1.0. Hivyo mfumo huu mpya haukupata umaarufu vile.
Kipindi cha miaka mitano baadaye Microsoft ilitoa mifumo mipya ya Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi kuliko mifumo ya hapo awali. Kampuni ya Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi katika soko la hisa, na akiwa umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa bilionea mchanga zaidi katika historia ya Marekani.
Katika mwaka wa 1990 Microsoft ikiongozwa na Bill Gates ilitoa toleo jipya la Windows liitwayo Windows 3.0 na kuboreshwa kiasi GUI. Toleo hili jipya liliweza kuuzwa zaidi ya nakala milioni kumi, likifuatiwa na matoleo mengine ya Windows 3.1, 3.11 na makundi ya kazi ambayo yaliongeza misaada kwa mitandao. Kutokana na mafanikio yao ya maendeleo, Microsoft ilitoa matoleo mengine ya Windows 95 ikifuatiwa na Windows 98, 2000, Millennium Edition na toleo la sasa Windows XP. Kila toleo jipya lilipotolea kampuni ya Microsoft ilizidi kupata umaarufu katika soko la hisa, ikiongezwa na baadhi ya programu kama vile Microsoft Office, michezo n.k. Umaarufu huu umemfanya Bill Gates kuwa mtu tajiri duniani myenye thamani ya wastani wa dola bilioni arubaini na sita.
Bill Gates pia ana maslahi katika biashara nyingine akiwa na nafasi nyingi za uwekezaji na vyeo katika kampuni tofauti ikiwemo Corbis Corporation, Berkshire Hathaway Inc, Teledesic Corporation. Mwaka wa 1998 Gates alijitoa jukumu lake kama Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Microsoft na kuzingatia maendeleo ya teknolojia na bidhaa mpya.
Bill Gates alifanya ndoa na Melinda French Gates mwaka wa 1994 na wakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na Fibi. Wote wawili Bill na Melinda ni waanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Waliweza kulianzisha shirika la Bill na Melinda Gates Foundation ambalo limeweza kuchangia zaidi ya dola bilioni tatu nukta mbili kuboresha afya duniani, dola bilioni mbili kuboresha fursa ya masomo kwa familia zisizojiweza. Zaidi ya hayo limeweza pia kuchangia dola milioni mia nne sabini na saba kwa miradi ya jamii na zaidi ya dola milioni mia nne themanini na nane kwa miradi maalum na kampeni za kuhamasisihwa kila mwaka.
Ubunifu wa Bill Gates wa kutengeneza programu umekuwa mchango wake katika mapinduzi ya kompyuta na sayansi ya kompyuta.

Sunday 29 December 2013

Yerusalemu

Yerusalemu

Yerusalemu
Jerusalem Dome of the rock BW 13.JPG
Ukuta wa Maombolezo na Kuba ya Mwamba mjini Yerusalemu
Emblem of Jerusalem.svg
Seal
Flag of Jerusalem.svg
Flag
Jina laKiebraniaיְרוּשָׁלַיִם (Yerushalayim)
Jina laKiarabuالقـُدْس (al-quds);
rasmi: أورشليم القدس
(urshalim-al-quds)
Maana ya JinaKiebrania: "Urithi wa amani",
Kiarabu: "(Mji) mtakatifu"
UtawalaMji
Wilaya
Wakazi724,000 (Wayahudi 68%, Waislamu 30%, Wakristo 2%) (2006)
Eneo126,000  (126 km²)
MeyaNir Barkat
Tovuti rasmiwww.jerusalem.muni.il
Yerusalemu (mara kwa mara pia Kudisi) (kwa Kiebrania ירושלים Yerushalayim, kwa Kiarabu: القدس al-Quds) ni mji wa Mashariki ya Kati wenye pande mbili. Kwa upande mmoja ni mji mkuu wa Israel. Kwa upande mwingine Yerusalemu ya mashariki inatazamiwa kuwa mji mkuu wa Palestina ingawa imetawaliwa na Israel pia tangu 1967. Israel imetangaza tangu 1980 Yerusalemu yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi za dunia hazikubali azimio hili hivyo balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Yerusalemu.
Yerusalemu ina historia ndefu sana. Ni mji muhimu katika dini tatu zinazofuata imani ya Abrahamu, yaani UyahudiUkristo na Uislamu.
BlankAsia.pngMakala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Yerusalemu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Saturday 21 December 2013

P FUNK

P. Funk

Paul Majani
P Funk Majani.jpg
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwaPaul Matthysse
Pia anajulikana kamaP Funk, Majani, Kinywele Kimoja, Mdachi nk.
Asili yakeTanzania
Aina ya muzikiHip Hop na Bongo Flava
Kazi yakeMtayarishaji
AlaKinanda,Guitar, Kinakilishi
Miaka ya kazimn. 1995 -
StudioBongo Records
Ame/Wameshirikiana naMaster JayBonny Luv,Rajabu Marijani,Bizz Man, Boznia nk.
Paul Matthysse ( P Funk ) ni mtayarishaji wa muziki na pia mmiliki wa Studio ya Bongo Records iliyopo jijini Dar es SalaamTanzania. P Funk ambaye nusu Mtanzania nusu Mdachi, kama miaka ishirini iliyo pita hivi .P Funk a.k.a Majani, alikuwa na hisia za kupendelea muziki na pindi hadi kuamua kufanya kweli.. kuvutiwa kwake kupenda muziki ndio chanzo kikumbwa.. kilicho pelekea kufanikiwa vizuri katika muziki.
Kwenye Miaka 1991-92 wakati yupo bado shule IST (International School Of Tanganyika. Alikuwa mtundu mtundu kwenye studio za pale shule.. kupiga- piga midundo mbali mbali ya hapa na pale na kufoka-foka(Rap music) na pia alikuwa mbele sana kwa kupiga musiki kwenye Pati mbali mbali.. na hapo alikuwa kupenda sana musiki kwa ujumla.

Elimu ya Muziki na Uzoefu Wake[hariri]

P-Funk alikwenda kimasomo ya Mlio (sound) engineering kwa miezi 18 pale AmsterdamNetherland kabla ajaingia kwenye kutayarisha muziki. Alikuwa anajua kitu anachotaka kufanya. Mwaka 1995 akiwa na vifaa vyake vichache alianzisha kampuni yake ya kurekodi muziki nyumbani kwake. Na ni katika kipindi hicho hicho neno ’Bongo’lilipokuwa linatawala katika misemo ya kiswahili cha mitaani na lilikuwa linaelezea hali halisi ya maisha ya Dar es Salaam na ndio kipindi hicho album ya Bongo ilipozinduliwa. Akiwa bado ni mtayarishaji muziki mdogo, amefanikiwa kupata umaarufu mkubwa katika fani ya muziki na hasa katika milipuko ya nyimbo zenye ladha ya Bongo.
Anakubali kuwa amepata sana utaalam na mbinu kutokana na kufanya kazi watayarishaji wengine wa muziki wa Kitanzania kama Master J, Bonny Love na Rico. Mawazo yake na namna ya kuyaoainisha na muziki ndio hasa ambacho kinafanya muziki wake ufanikiwe.

Tuzo Alizopata[hariri]

Wasanii Aliowainua[hariri]

Kwanza alianza kwa kumpandisha chati Juma Nature ambaye ndio nyota wa nyimbo za Bongo Flava na akaendelea kwa kutayarisha santuri yaSolo ThangAYZay BSista PMike T na pia alishawahi kufanya kazi na Professor Jay alipotoa santuri yake mwenyewe. P Funk ana wasanii wengine wengi wanaotumia nembo ya kampuni yake katika Utengenezaji wa albamu.

Pia Anajulikana Kama[hariri]

  • P Funk
  • Halfani
  • Majani
  • Kinywele Kimoja
  • Mkono wa mungu
Musical notes.svgMakala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu P. Funk kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
safi sana

Sunday 15 December 2013

HISTORIA YA George Washington

George Washington

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Washington akisimamia shamba na watumwa.
Washington akivuka mto Delaware katika vita ya uhuru ya Marekani.
Sanamu ya Washington pamoja na maraisi wengine kwenye mlima Rushmore
Nyumba yake kwenye shamba la Mount Vernon
Washington kwenye pesa la Marekani.
George Washington (22 Februari 1732 hadi 14 Desemba 1799) alikuwa mwanasiasa, kiongozi wa kijeshi na rais wa kwanza wa Marekani kati ya 1789 na 1797.

Mtoto na kijana[hariri]

Alizaliwa kama mtoto wa pili wa mlowezi Augustine Washington katika koloni ya Virginia iliyokuwa mali ya mfalme wa Uingereza. Wazazi walikuwa na shamba kubwa lililolimwa na watumwa Waafrika. George alisoma shule miaka michache hakuendelea sana kielimu. Baada ya shule alianza kazi ya upimaji na ramani.

Mkulima na kiongozi wa kijeshi[hariri]

Baada ya kifo cha kakaye alirithi shamba kubwa pamoja na watumwa akawa mkulima mtajiri. Sehemu ya urithi ilikuwa cheo cha msimazi wa wanamgambo waliokuwa kikosi cha kijeshi cha hiari waliotakiwa kusaidiana na wanajeshi Waingereza kutetea koloni dhidi ya majirani Waindio na Wafaransa walioenea kuelekea kusini kutoka koloni yao ya Kanada - Quebec.
Katika umri mdogo wa miaka 22 Washington alijikuta kama mkuu wa wanamgambo katika vita ya Uingereza dhidi ya Wafaransa na Waindio iliyopanuka baada ye kuwa Vita ya Miaka Saba. Akaongoza kikosi chake dhidi ya maadui akafaulu mara kadhaa. Baadaye alishirikiana na jeshi rasmi la Uingereza katika mapigano ya Monongahela na kuongoza mabaki ya jeshi baada ya kifo cha jemadari Mwingereza. 1755 akawa mkuu wa jeshi la koloni Virginia. Lakini baada ya ushindi Waingereza walikataa kumpa cheo katika jeshi la mfalme hivyo akajiuzulu akirudi kwa shamba lake na kufuata siasa kwenye bunge la koloni.
1759 Washington akamwoa mjane mtajiri akawa kati ya matajiri kabisa wa Virginia.

Mapinduzi[hariri]

Baada ya vita ya miaka saba uhusiano kati ya Uingereza na walowezi Waingereza katika koloni zake 13 za Amerika ya Kaskazini ukazorota. Tangu 1773 Waingereza walitumia sheria ya dharura na nguvu ya kijeshi mjini Boston. Wawakilishi wa koloni zote 13 wakakutana kama bunge la Amerika Bara na Washington alikuwa miongoni mwao.
Baada ya mapigano ya kwanza kati ya wanajeshi Waingereza na wanamgambo wa walowezi bunge likaamua kuunda jeshi la pamoja la koloni zote na Washington akateuliwa kuwa jemadari mkuu.
Aliongoza jeshi la Marekani katika vita ya uhuru wa Marekani dhidi ya Uingereza hadi mwaka 1783.

Baada ya vita: mwanasiasa na rais[hariri]

Baada ya vita ya uhuru ya Marekani Geroge Washington akarudi kwake akalima tena lakini akachaguliwa pia kama mwakilishi wa Virginia katika bunge la katiba la Marekani mwaka 1787 akawa mwenyekiti wa mkutano huu uliokubali katiba ya Marekani.
4 Februari 1789 alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani akirudishwa mwaka 1789. Baada ya kipindi chake cha pili alikataa kusimama tena akaunda hivyo utaratibu ya kwamba rais anaweza kurudishwa mara moja tu hawezi kuendelea zaidi.

Uzee[hariri]

1797 akarudi tena kwake shambani aliposimamia kilimo kilichoendeshwa na watumwa 390. Tar. 14 Desemba alikufa kwake nyumbani. Kabla ya kuaga dunia aliamuru katika usia wake ya kwamba watumwa wake wote warudishiwe uhuru baada ya kifo chake yeye mwenyewe na mke wake.
Mji mkuu wa Marekani Washington, D.C. na jimbo la Washington vimepokwa majina kutokana naye. Picha yake iko kwenye noti ya dollar moja.