member

NYEPESINYEPESI

          PELE AUSHANGAZA ULIMWENGU

KATIKA KUCHAGUA MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA WAKIWA WAMEKUSANYIKA MAKOCHA NA WACHEZAJI WENYE MAJINA WA SASA NA WA ZAMANI AKIWEMO PELE,NEYMAR ,RONALDO,MESSI.

BAADA YA KIKAO KUISHA .KIONGOZI WA MKUTANO AKAAMUA KUANZISHA HOJA BINAFSI ILI WATU WAPIGE KURA NA APATIKANE MSHINDI,KUMBUKA MULE NDANI IDADI KAMILI YA WATU WOTE ILIKUWA MIA MBILI.KIONGOZI AKAULIZA SWALI ""KATI YA NEYMAR NA MESSI NANI MKALI "" WAKATI WATU WANAJIULIZA CHINI KWA CHINI ILI WATOE MAJIBU KAMILI MARA PELE AKAAMKA NA KUSEMA ""NEYMAR MKALI NA IMEPITISHWA HAMNA MASWALI'''' KIONGOZI AKAONA WATU WAMENYAMAZA KIMYA KWA KUSHANGAZWA NA MAJIBU YA PELE AKAAMUA AULIZE SWALI LINGINE ""KATI YA RONALDO NA NEYMAR NANI MKALI""" PELE AKANYANYUKA TENA KWA KISHINDO HUKU AKICHEKA KABISA AKASEMA ""NEYMAR MKALI NA IMEPITISHWA HAKUNA MASWALI "" WATU ILIBIDI WABAKI WAMESHANGAA

        NITAWAITA KWA UBINI WA BABA YAO 

JAMAA MMOJA NCHINI CHINA AMEITA MKUTANO WA VYOMBO VYA ABARI NAKUSHAURI NAMNA MPYA YA KUTOA MAJINA,AKASEMA'' KWA SASA MTU UNATAFUTA JINA LA KUWAPA WANAO UNAKOSA CHA MSINGI UKIWA NA WATOTO ZAIDI YA WATANO WAITE TU JINA MOJA LINATOSHA YAHANI MFANO MIMI WANANGU NITAWAITA JUNG LEE'' AKAULIZWA KAMA WAMEKAA PAMOJA UTAWAITAJE AKASEMA NI RAHISI NITAWAITA KWA UBINI WA BABA YAO,WAANDISHI WA HABARI IKABIDI WASHIKWE NA BUMBUWAZI KWANI BABA MWENYEWE NDIO HUYOHUYO

KUTOKUJUA  SHERIA NALO NI KOSA KISHERIA

  JAMAA MMOJA AMEJIKUTA AKIPATA KIFUNGO CHA MWAKA MZIMA BILA KUKUSUDIA KUPATA HICHO KIFUNGO.HAYO YAMETOKEA KWENYE MAHAKAMA KUU JIJINI DARESSALAAM MARA BAADA YA JAMAA HUYO KUJIFANYA KIHERERE WA KUHUDHURIA MAHAKAMANI BILA KUJUA TARATIBU ZA MAHAKAMA.HAKIMU ALIINGI WATU WAKIWA WAMEKAAA NDIPO ILIPOSEMWA COURT WATU WOTE WAKASIMAMA KASORO JAMAA MWENYE KIHEREHERE.HAKIMU PALEPALE KABLA AJASIKILIZA KESI AKAMTWANGA JAMAA JELA KIFUNGO CHA MIEZI SITA,KISHA HAKIMU AKAMWAMBIA JITETEE,JAMAA AKASEMA NAOMBA MNISAMEHE KWANI NILIKUWA SIJUI SHERIA,PALEPALE HAKIMU AKATOA HUKUMU NYINGINE KWA KUMTWANGA TENA MIEZI SITA MINGINE KWA KUTOJUA SHERIA ,BAADA YA HAPO POLISI WALIKUJA KUMCHUKUA KUMPELEKA JELA  

 

         JOTI AHARIBU SWALA MSIKITINI


KATIKA ILE HALI YA KUTOMTII KIONGOZI WAKO UNAWEZA UKAPATA MADHARA IMEWAKUTA WAISLAMU KATIKA MSIKITI MMOJA ULIOPO KATIKA VIUNGA VYA JIJI LA DARESSALAAM.BAADA YA IMAMU KUWAAMBIAWAUMINI WAZIME SIMU. WAUMINI WAKAZIMA KUNAMMOJA HAKUZIMA.WAKIWA NDANI YA YA SWALA SIMU IKAITAKWA MLIO WA JOTI ''MMH ZIRA WE MUONGO ZIRA WAZUNGU UNAWAJUA'' MLIO HUO ULISABABISHA KARIBIA NUSU YA SAFU YA KWANZA KUCHEKA HIVYO SWALA ZAO KUHARIBIKA.JAMAA YULE ILIBIDI AOMBE LADHI LAKINI WATU HAWAKUMUELEWA WAKAMCHARAZA BAKORA.JAMANI HII NI TANBIHII KWA WOTE MSIO WATII VIONGOZI WENU MUWATII



MWANAUME MWENYE WAKE WAWILI AMLAWITI MTOTO WA MIAKA 6

KATIKA kile kinachoonekana kama kuishiwa utu, mwanamume mmoja mwenye wake wawili, mkazi wa Kitongoji cha Kampaundi, Kijiji cha Nyamalembo katika Kata ya Mtakuja, Wilaya ya Geita, anatuhumiwa kumuingilia kinyume na maumbile mtoto wa kike wa miaka sita.
Kitendo hicho kimeelezwa kumsababishia maumivu makali mtoto huyo hatua ya kumfanya atokwe na kinyesi mfululizo.

Mtoto huyo aliyefanyiwa ukatili huo (jina linahifadhiwa), kwa sasa anauguza majeraha aliyosababishiwa na mwanaume huyo, aliyefahamika kwa jina moja la Mchuchu (26) ambaye ni jirani yao.Tukio hilo limetokea Julai 7 mwaka huu katika moja ya vyumba vya jengo linalotumika kama Ofisi ya Serikali ya Kijiji hicho ambamo pia kuna ofisi ya Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Sabuni Makima.

Akithibitisha tukio hilo, Makima alisema kuwa tayari ofisi yake imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kushirikiana na jeshi la polisi kumsaka mtuhumiwa hadi apatikane na kufikishwa mahakamani.
“Huyu bwana ni muuaji kabisa…nasi kama serikali hatuwezi kukubali kuona anaendelea kutanua wakati amemuathiri kisaikolojia huyu mtoto na kumpatia maumivu. Tumeunda kikosi kazi kitakachosaidiana na polisi kumsaka huyu mtuhumiwa,” alisema Makima.

Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa lilitokea majira ya saa 10 jioni wakati mama mzazi wa mtoto huyo akiwa amefuata maji kisimani. Mama wa mtoto huyo, Evelina John (32), aliwaambia waandishi wa habari kuwa aliondoka kwenda kisimani kuteka maji na kumwacha mwanaye huyo na wadogo zake wakiangalia maharage yaliyokuwa yakipikwa jikoni.
“Wakati niliporudi nilishangaa kumuona mwanangu mwingine, Anjelina (4) akiwa pekee yake huku akielekea juu mlimani, ndipo niliamua kumuita na kumhoji aliko dada yake, akaniambia kuwa amemuacha kwa Mchuchu.

“Nilipomuuliza tena alipo dada yake, alidai kuwa amefungiwa ndani na Mchuchu na amelazimishwa kufagia chumba chake…kwa kweli taarifa hizo zilinishtua ukizingatia kuwa nilikuwa nimemuachia maharage yalinde yasiungue na bila kuchelewa nilikwenda moja kwa moja hadi huko,” alisema.
Mama huyo alifafanua kuwa alipofika kwa mtuhumiwa huyo alikuta mlango wa chumba chake ukiwa umefungwa kwa ndani na hata alipogonga hakuitikiwa.
“Niliamua kumuita mtoto wangu Anjelina na kumuagiza amfuate baba yake aliyekuwa amelala nyumbani ili naye aje anisaidie kutatua suala hilo nami niliendelea kubaki mlangoni ili nione kinachoendelea,” alisema.

Evelina alisema kuwa kitendo cha kumuagiza mtoto amfuate baba yake kilimshtua Mchuchu na hivyo alichomoka kupitia dirishani na kukimbia kusikojulikana akiacha amefungua komeo la mlango wa chumba alichokuwa akifanyia unyama huo.“Kwa kweli tulichokishuhudia baada ya kuingia ndani kilituogopesha sana na sikutegemea kwamba mwanaume huyo mwenye wake wawili angeweza kumfanyia mtoto wangu unyama kama ule, alisema.

Aliongeza kuwa walimkuta mtoto huyo akiwa ametapakaa kinyesi mwili mzima na walipomuuliza alidai kwamba alikuwa amefungwa kitambaa cheusi usoni na mdomo wake ulijazwa matambala na kuzungushiwa kamba ngumu za waya ili asiweze kufungua kamba hizo na kupiga kelele.
Mtoto huyo aliwaeleza kuwa kisha alifungwa kamba mikononi na baadaye Mchuchu alimpanua miguu yake akaining’iniza kwa juu na kuanza kumwingilia kinyume na maumbile.
“Niliposikia hivyo, nililia kwa uchungu kelele ambazo ziliwashtua majirani ambao walikusanyika eneo la tukio akiwemo balozi wetu wa nyumba kumi, Jackson Mtalemwa, na walipofika na kumushuhudia mtoto wetu alivyokuwa ameumizwa walitushauri kumuwahisha polisi ili tupatiwe fomu ya matibabu (PF3),” alisema.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo, hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo kwa maelezo ya wasaidizi wake kuwa alikuwa nje ya ofisi kikazi.

Matatizo ya ubakaji yanaendelea kukua licha ya sheria kali zilizowekwa. hapa tatizo sio sheria kali ila inaonyesha jinsi shetani anavyotumia nguvu kama akipewa nafasi. wapendwa tuendelee kuomba kuna vitu vingi sana ambavyo haviendi sawa ambavyo naamini mtu wa Mungu unapaswa kuviombea ili viende sawa.

KIPIGO CHA DK ULIMBOKA CHAWA SEHEMU YA KUTISHANA JAMAA AAMA MAKAZI KWA MUDA


Baada ya gazeti moja kutoa namba ya mtu anaesadikiwa kuwa ndiye aliempiga Dr ulimboka jamaa mmoja mwanye tabia ya kujaribujaribu mambo kwa sifa mkoani Tanga maeneo ya makorora alijaribu kumpigia simu alipompigia simu mara ya kwanza mzee wa kujaribu mambo alijifanya ananyadhifa za juu usalama wa taifa lakini ghafla yule jamaa akakata simu,Jamaa zake wakalibu yule bwana mpenda sifa wakatafuta line mpya ya airtel wakajaza pesa alafu wakampigia jamaa wao ambaye alikuwa tigo wakamwambia haya mimi ndiye niliyempiga ulimboka sema unachotaka ukusema jamaa akiwa anataka kujipandisha vyeo jamaa wakamwambia sisi ni watu wa usalama na tutakufata popote ulipo,alafu wakamwambia unakaa wapi ,jamaa akajifanya anakaa chumbageni,jamaa wakamwambia wewe unatudanganya wewe unakaa makorora na wewe ni mrefu mweusi na unaitwa Saidi jamaa mpenda kujaribu mambo akajikuta anaomba msamaha samahani mzee ni ujinga wangu tu,jamaa wakazidi kumtisha wakamwambia nyinyi ndio mnaotuma kufatilia infomation za nchi jamaa akazidi kulia kwa unyenyekevu huku akisema samahani mzee ni ujinga wangu,jamaa wakamwambia hata ukizima simu tutakufata tu sisi tunajua mpaka unapokunya ,baada kukata simu jamaa akaenda kukata tiketi a zanzibar akajifiche wenzake walivyoona anafikia mbali wakamwambia walimtisha jamaa akamind sana kwani kashalipa tiketi.hili ni onyo kwa viherehere




JITU KUBWA LAWASHANGAZA ABIRIA KWENYE DALADALA





Lipota wetu akiwa kwenye basi inayotoka ubungo kuelekea mbagala alishuhudia mzozo ndani ya basi hasa baada ya konda kutomwambia dereva awashushe sheli maeneo ya buguruni na akawapeleka mpaka chama kituo kilichofata,watu walishuka huku wakiwa wanamtukana konda kwa kuwapitisha kituo,katika hali isiyo ya kawaida JITU KUBWA lilionekana kukerwa na kitendo cha yule konda likiwa limekaa siti ya mwisho liliwaomba abiria wampishe,huku akionekana ni mwenye jazba na watu wakategemea kitendo kinachofata ni konda kupigwa ngumi na JITU KUBWA ,lilienda mbele pale aliposimama konda ,Abiria wote walikaa kimya waone nini kitatokea maana JITU KUBWA lilikuwa limekunja uso,Konda naye aliingiwa woga na kuanza kutamani kuomba msamaha maana alikuwa hajui JITU KUBWA .Litamfanya nini ,katika hali isiyo ya kawaida JITU KUBWA lilimfata konda na kumuangalia kama bondia mrefu anapomuangalia bondia mfupi kisha likasema yafuatayo "konda ndevu kama za mbuzi anamzuzu lakini anakula majani" Kisha likashuka watu ilibidi wabaki na kicheko maana waliyoyategemea kwa JITU KUBWA siyo matokeo yake wameshuhudia mambo ya kitoto





No comments: