member

Thursday 28 November 2013

Kieran Gibbs

Kieran Gibbs

Rukia: urambazaji, tafuta
Kieran Gibbs
Gibbs, Kieran (1).jpg
Maelezo binafsi
Jina kamili James Ricardo Kieran Gibbs
Tarehe ya kuzaliwa 26 Septemba 1989
Mahala pa kuzaliwa    Lambeth, London, Uingereza
Urefu 1.80 m (5 ft 11 in)
Nafasi anayochezea Difenda
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Arsenal
Namba 28
Klabu za vijana
2001–2004
2004–2007
Wimbledon
Arsenal
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2007– Arsenal
Norwich City (mpango wa mkopo)
Timu ya taifa
2007–2009 Uingereza
* Magoli alioshinda

Historia

James Ricardo Kieran Gibbs (alizaliwa 26 Septemba 1989) ni mchezaji wa kandanda wa Uingereza ambaye huchezea timu ya Arsenal kama mchezaji wa nyuma. Yeye alihudhuria Shule ya Upili ya Riddlesdown katika eneo la Purley,Kusini mwa London.

Wasifu

Wasifu wa Klabu

Gibbs alianza kazi yake katika shule ya Wimbledon lakini akahamia Arsenal ,pamoja na Abu Ogogo na James Dunne, Wimbledon ilipoachishwa kazi katika mwaka wa 2004 na ikawa Milton Keynes Dons. Yeye alicheza katika nafasi ya kati na pia kwenye upande wa kushoto. Yeye alihusika mara kwa mara katika timu ya Arsenal ya vijana walio chini ya umri wa miaka 18 na timu hifadhi.Alicheza pia mechi za kirafiki dhidi ya Barnet na Inter Milan. Mnamo Septemba 2007, Gibbs alitia saini mkataba na Arsenal, na alikuwa mmojawapo katika timu iliyotajwa kucheza katika msimu wa 2007-08 Ligi ya Mabingwa ya UEFA na akapewa jezi nambari 34.
Yeye alichezea timu rasmi ya Arsenal kwa mara ya kwanza alipoashiriki katika mechi ya Shindano la Kombe la League dhidi ya Sheffield United mnamo 31 Ktoba 2007.Alicheza tena ,kwa mara ya pili, alipoingia kama mchezaji mbadala wa Eduardo da Silva katika robo fainali dhidi ya Blackburn Rovers,18 Desemba 2007.
Tarehe 31 Januari 2008, yeye alikubali mpango wa mkopo ambao angeenda kucheza katika timu ya Norwich City hadi mwisho wa msimu wa 20007-08. Yeye alirudi Arsenal mwanzoni mwa mwezi wa 29 Aprili 2008 na akachukua nafasi yake katika timu hifadhi ya Arsenal> Yeye alikwenda na kuchaguliwa kama mchezaji mbadala wa kuingia kucheza katika mechi dhidi ya Everton mnamo 4 Mei 2008 lakini hakucheza.
Alicheza katika mechi za kabla ya msimu wa 2008-09,mara nyingi akicheza kama difenda kule nyuma, na akawa mchezaji ambaye hakutumiwa katika mechi dhidi ya Fulham walioshindwa 1-0,24 Agosti 2008, na pia hakutumiwa katika ushindi wao dhidi ya Bolton Wanderers wa 3-1(Septemba). Gibbs aliendelea kucheza katika Shindano la Kombe la League na akacheza dakika 90 katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Sheffield United katika raundi ya tatu ya mechi,23 Septemba 2008. Yeye,pia, alicheza waliposhinda 3-0 dhidi ya Wigan Athletic na vilevile alicheza katika mechi ya kushindwa dhidi ya Burnley katika hatua ya robo fainali. [14] [15] [16] Yeye alicheza kwa mara ya kwanza katika Shindano la Ligi ya Mabingwa ya UEFA mnamo 10 Desemba 2008 dhidi ya Porto FC akiwa mchezaji mbadala wa Abou Diaby.
Gibbs alicheza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu Ya Uingereza dhidi ya Tottenham Hotspurs mnamo 8 Februari 2009 akiingia kama mchezaji mbadala wa Gael Clichy aliyeumia katika mechi hiyo.
Gibbs katika mazoezi
Clichy akiwa ameumia, Gibbs alianza mechi yake ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa katika robo fainali dhidi ya Villareal mnamo 15 Aprili 2009,Arsenal ilishinda 3-0. Gibbs alianza kucheza mechi ya Shindano la Kombe la FA dhidi ya Chelsea na akamsaidia Theo Walcott kufunga bao. Alihusika ,pia, wakati Arsenal na Liverpool walipotoka sare dhidi ya Liverpool, 21 Aprili, huko Anfield.Aliokoa timu yake kwa kupiga mpira ulipokuwa karibu kuingia goli.
Baada ya kucheza mechi mingi katika timu rasmi kwa kuwa Clichy alikuwa ameumia, Gibbs alicheza katika nusu fainali ya Shindano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United,Arsenal walishindwa 1-0. Hata hivyo, katika mkondo wa pili wa mnusu fainali hiyo, Gibbs alifanya kosa lililomwezesha Park Ji-Sung kufunga bao muhimu sana baada ya dakika 7. [21]
Alianza katika mchuano wa kwanza wa Arsenal wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Portsmouth na akacheza dakika 90. Clichy alipojeruhiwa na kutoweza kucheza kwa wiki kadhaa,Arsene Wenger alimpa Gibbs nafasi katika timu. Hata hivyo,mnamo tarehe 24 Novemba, Gibbs alivunjika mfupa mguuni katika mechi dhidi ya Standard Liege na jeraha hili likamtoaa kwa mchezo kwa wakati usiojulikana,Arsenal ilishinda 2-0.

Wasifu wa Kimataifa

Yeye alikuwa katika timu ya Uingereza ya vijana wa chini ya umri wa miaka 19 ambayo ilishindwa katika mkondo wa vikundi katika Shindano la UEFA la 2008 la vijana wa chini ya umri wa miaka 19.Hata hivyo, walihitimu kucheza katika Shindano la Kombe la Dunia la vijana wa chini ya umri wa miaka 20 nchini Misri lililoandaliwa na FIFA.
Gibbs aliitwa kujiunga na kikosi cha Uingereza cha vijana wa chini ya umri wa miaka 21 akiwa pamoja na mwenzake kutoka Arsenal ,Theo Walcott.Walichaguliwa ili wacheza katika shndano la Uropa la 2009 la vijana wa chini ya umri wa miaka 21 nchin Uswidi. Yeye alifunga mabao mawili katika mchuano wa kirafiki na Azerbaijan kabla ya shindano mnamo 8 Juni 2009,walishinda 7-0.Alifunga mkwaju wake wa penalti katika nusu fainali ya shindano hilo dhidi ya Uswidi.
Stuart Pearce alimworodhesha Gibbs katika mechi za kuhitimu kucheza katika shindano la Mabingwa wa Uropa ya 2011. Yeye alifunga bao la kwanza katika ushindi wao wa 6-3 dhidi ya Masedonia hapo 9 Oktoba.

Takwimu ya Wasifu

(sahihi 24 Novemba 2009)
Klabu Msimu Ligi Kombe la FA Kombe la League Uropa Jumla
Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi wa kufunga bao
Arsenal 2007–08 0 0 0 0 0 0 2 0 1 0 0 0 2 0 1
Norwich City (mpango wa aina ya mkopo) 2007–08 7 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 0 7 0 0
Arsenal 2008-09 8 0 0 6 0 1 3 0 1 4 0 0 21 0 2
Arsenal 2009-10 3 0 0 0 0 0 2 0 0 2 0 1 7 0 1
Jumla 18 0 0 6 0 1 7 0 2 6 0 1 37 0 4

Tuzo

Arsenal FC

IKimataifa

  • Nafasi ya pili katika Shindano la Mabingwa ya UEFA kwa vijana walio chini ya umri wa 21(2009)

Binafsi

Marejeo

  1. ^ Gibbs and Dunne delighted by pro contract, arsenal.com,
  2. ^ "2007/08 UEFA Champions League - Matchweek Stats Pack". UEFA. http://www.uefa.com/printoutfiles/competitions/ucl/2008/e/e_01_md.pdf.
  3. ^ "Sheff Utd 0-3 Arsenal". BBC Sport. 2007-10-31. http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/league_cup/7065196.stm..
  4. ^ Arsene Wenger’s conveyor belt of talent shows no sign of slowing down, timesonline.co.uk,
  5. ^ Blackburn 2-3 Arsenal (aet), bbc.co.uk,
  6. ^ Sky Sports | Football | Premier League | Arsenal | Canaries swoop for Gibbs
  7. ^ Reserves: Aston Villa v Arsenal - Preview
  8. ^ Arsenal.com
  9. ^ "Fulham 1-0 Arsenal". Arsenal.com. http://www.arsenal.com/match-menu/3003005/first-team/fulham-v-arsenal?tab=report.
  10. ^ - Arsenal 6-0 Sheff Utd, BBC Sport,
  11. ^ - Arsenal 3-0 Wigan , BBC Sport,
  12. ^ - Burnley 0-2 Arsenal , BBC Sport,

Viungo vya nje

Sunday 24 November 2013

historia ya Joshua Nkomo

oshua Nkomo

Rukia: urambazaji, tafuta
Joshua Nkomo.
Joshua Mqubuko Nyongolo Nkomo (19 Juni 1917[1]1 Julai 1999) alikuwa mwananisiasa, kiongozi na mwanzilishi wa chama cha Zimbabwe African People’s Union na pia ni mtu wa kabila la Kalanga[2] kutoka nchini Zimbabwe. Huyu alikuwa anajulikana kama baba wa Zimbabwe au katika Lugha ya Zimbabwe ‘’umdala Wethu, Umafukufuku au chibwechitedza’’ jiwe linaloteleza au (the slipery rork)

Maisha ya awali

Nkomo alizaliwa katika sehemu ya Somokwe katika ardhi ya Matebel mwaka 1917, katika familia ya watoto nane. Baba yake alikuwa anaitwa Thomas Nyongolo Letswansto Nkomo, aliokuwa akifanya kazi kama mchungaji na pia alikuwa ni mfanyakazi katika Chama cha Kimishonari cha London au London Missionary Society. Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi katika jimbo la Rhodeshia alijifunza masomo ya ufundi useremala katika shule ya Viwanda ya Tsholotso ambapo alisoma hapo kwa muda wa mwaka mmoja na baadae akawa dereva. Baadae alifanya kazi kama mfugaji na baadae akawa mwalimu na alikuwa mahususi katika maswala ya useremala katika shule ya Manyame katika jimbo la Kezi. Mwaka 1942, akiwa na miaka 25, na bado akiwa na kazi yake kama mwalimu, aliamua kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo na hatimaye kuwa fundi seremala mahususi. Alijiunga na chuo cha Adams na Chuo cha Ufundi cha Jan Hofmeyer nchini Afrika ya Kusini. Akiwa hapo alikutana na Nelson Mandela na viongozi wengine mbalimbali waliokuwa katika chuo kukuu cha Fort Hare University of Fort Hare japokuwa hakuwa akisoma katika chuo kikuu hicho. Ni katika chuo cha ufundi cha Hofmeyr.Hofmeyr School of Social Work ambapo ndipo alipopata shahada yake ya kwanza katika maswala ya Sayansi ya Jamii mwaka1952.

Ndoa

Nkomo alimuoa Mke wala anaitwa Johanna Mafuyana tarehe 01/10/1949. Baada ya kurudi kutoka Bulawayo mwaka 1947, alikuwa moja kati ya wapigania haki wafanyakazi wa shirika la Reli na Baadae kuwa kiongozi wa Umoja wa wafanyakazi wa Reli na baadae kuwa kiogozi wa African National Congress mwaka 1952. Mwaka 1960, alikuwa raisi wa chama cha National Democratic Part ambacho baadae kilifungiwa na serikali ya Rhodesia. Pia Nkomo amekuwa ni moja kati ya wajasiriamali matajiri zaidi katika eneo la Rhodesia.

Mapinduzi ya Silaha

Nkomo alitiwa Kizuizini katika kambi ya Gonakudzingwa na serikali ya Ian Smith mwaka 1964, wanamapinduzi wenzake kamam vile Ndabaningi Sithole, Edger Tekere Maurice Nyagubo na Robert Mugabe hadi mwaka 1974, lakini baadae waliachiwa baada ya shinikizo kutoka na Raisi wa Afrika ya Kusini.during the apartheid eraSouth African B.J.Vorster. Baada ya Kuachiwa, Nkomo alienda nchini Zambia kuendelea na mapambano ya chini chini na pia majadiliano. Tofauti na ZANU yaani (Zimbabwe African National Liberation Army) na mapambano ya silaha , chama cha ZAPU (Zimbabwe people’s Revolution Army) kilikuwa kimeamua kufanya mapambano ya msituni na mazungumzo. Katika kipindi cha uhuru, ZIPRA ilikuwa na silaha za kijeshi za kisasa na zilizokuwa zimehifadhiwa katika nchi za Zambia na Angola iliyokuwa pamoja na silaha nyingine za kivita kulikuwa na mizinga ya vita na wafanyakazi wa kisasa katika matumizi ya vifaa ivyo.

Jaribio la Kuuwawa

Joshua Nkomo alikusudiwa kufanyiwa mauaji mara mbili, mara ya kwanza ikiwa ni Nchini Zambia, lakini lengo hilo halikufanikiwa lakini pia lakini majaribio ya kumuua yalindelea na baadae yalifanywa na Rhodesia Special Air Service. Katika malengo hayo yalihusha nyumba aliyokuwa akiishi, kiongozi wa jaribio hilo alijaribu kuotroka lakini alikamatwa na mlinzi wa Nkomo akiwa amenaswa katika dirisha na bafuni. [3]. Majeshi ya ZAPU, yalifanya mambo mengi ya matumizi ya nguvua katika kuiondoa madarakani serikali ya Rhodesia. Moja kati ya mambo yanayasadikika kuwa ni ya kinyama zaidi kuwahi kutokea ni pamoja na mauaji katika ndege za abiria. Ya kwanza yalitokea tarehe 3/09/1978 na kuua watu 38, kati ya watu 56, na wengine kumi wakijeruhiwa, ikiwa ni oamoja na watoto. Waliobaki hai, walitembea kutoka kuotka eneo hilo hadi Kariba kiasi cha umbali wa kilometa 20. Baadhi ya wasafiri walikuwa wamejeruhiwa vibaya, ,na baadhi alichukuliwa na polisi wa jeshi la Rhodesia, Jaribio la pili lilikuwa tarehe 12/02/1979 na kuua watu 59, papo hapo, lakini malengo ya shambulizi la pili yalikuwa kwa ajili ya Peter Walls mkuu wa COMOPS (Commander Combined Operations) aliyekuwa anahusika na vifaa maalumu kama vile. Special Air ServiceSAS Walls alipokea tiketi ya kuondoka na ndege ya pili kutokana na idadi kubwa ya watalii, ndege ambayo iliondoka Kariba dakika 15, baada ya ndege iliyopotea. Hakuna mtu aliyeshitakiwa kwa makosa ya ndege kupotea kutokana na kutolewa kwa msamaha kutoka kwa Smith na Mugabe.
Katika mahojiano ya Televisheni, muda mfupi baada ya kupotea kwa ndege nyingine, ambapo, akiwa anacheka Nkomo alitania kuhusiana na matukio hayo na kuhakikisha kuwa ZAPU ndio wanaohusika na mashambulizi ya ndege mbalimbali. Katika vitabu vyake mbalimbali kama vile ‘’Story of my Life’’ kilichochapishwa mwaka 1985, Joshua Nkomo ameelezea masikitiko yake kuhusiana na mashambulizi ya ndege zote mbili

Siasa

200px-Nkomo-ZAPU.jpg
Nkomo alianzisha chama cha National Democratic Part (NDP) , na mwaka ambao waziri Mkuu wa Uingereza bwana Harold Macmillan alipoongelea “upepo wa mabadiliko” unavuma katika Afrika Robert Mugabe aliungana nae. Chama cha NDP kilifungiwa na serikali ya kibabe ya Smith na baadae chama cha Zimbabwe African People Union ZAPU ambacho pia kilianzishwa na Joshua Nkomo pamoja na Robert Mugabe mwaka 1962, kilichua nafasi ya NDP. Lakini pia kilizuiwa mapema. Chama cha ZAPU, kiligawanyika mwaka 1963, wakati wengine walihisi mgawanyiko huo ulikuwa ni kutokana na masuala ya Kikabila, lakini zaidi inaonesha kuwa mgawanyiko huo ulitokana na kushindwa kwa Sithole, Mugabe, Takawira na Malianga kuchukua madaraka ya ZAPU kutoka kwa Nkomo. ZAPU kikabaki chama chenye mjumuisho wa makabila mengi hadi kupatika kwa uhuru.
Serikali ambayo haikwa maarufu ilioyitwa Zimbabwe-Rhodesia ilioyokuwa inaongozwa na Abel Muzorewa iliundwa mwaka 1979kati ya Ian Smith na Ndabaningi Sithole’s . ZANU ambayo kwa wakati huo, ilikuwa tayari imeshagawanyika kutokana na Mambo ya kijeshi ya Mugabe. Lakini vita ilioyanzishwa na Nkomo na Mugabe viliendelea bila kupiganwa. Na Uingereza pamoja na Marekani havikuweka vikwazo katika nchi hiyo Uingereza ulivishawishi vyama hivyo kwenda katika Lancaster House mwezi wa tisa mwaka 1979, kwa ajili ya kuanzisha katiba na kuitisha uchaguzi upya. Mugabe na Nkomo walifanya makubaliano yaliyoitwa Patriotic Front (PF) katika makubaliano yaliyoendeshwa na Lord Carrington. Uchaguzi ulifanyika mwaka 1980, na katika macho ya wengi chama cha ZAPU kilichokuwa kinaongozwa na Nkomo kilishindwa katika uchaguzi huo na chama cha ZANU kilichoongozwa na Mugabe Matokeo ya uchaguzi huo. Yaliweka vyama vyote viwili ZAPU na ZANU katika vyama vinavyoegamia mfumo wa kikabila , yaani chama cha ZANU kikiwa na iadi kubwa ya ya kabila la Shona na chama cha ZAPU kikiwa na idadi kubwa ya kabila la Ndebele Nkomo alikaribishwa katika sherehe ya uraisi lakini alikataa.

Mapinduzi ya kijeshi

Hata baada ya kufikia lengo la kumwondoa Ian Smith na idadi kubwa ya wazungu.. bado Nkomo na Mugabe hawakuelewana. Nkomo alikuwa akijitahidi kuweka mahusiano mazuri katika vyama vyao viwili lakini Mugabe hakuwahi kuonesha ushirikiano kwani aliamini kuwa ZAPU kilikuwa na malengo ya kufanya mapinduzi na kukitoa madarakani chama cha ZANU. Wakati Julius Nyerere alipoviita vyama hivyo viwili katika mkutano uliokusudia kurejesha mahusiano mazuri, vyama hivyo viliingia katika ofisi ya Nyerere tafauti tofauti. Kwanza alianza Nkomo na kufuatiwa na Mugabe. Wakati Mugabe alipopewa kiti kwa ajili ya kukaa alimwambia Nyerere. "If you think I'm going to sit right where that fat bastard just sat, you'll have to think again" yaani “ kama unadhani naweza kukaa hapa na huyo mpumbavu alieakaa hapo, inabidi ufikirie tena” Kutoka na hali hiyo, mkazo uliongezwa kati ya mahusiano yao, mapigano kati ya chama cha ZANLA na ZIPRA yaliongezeka na kuongeza kutoelewana kati ya hawa watu wawili Hatimaye, baada ya majadiliano ya muda mrefu na kukataliwa mara kadhaa, Nkomo hatimaye alichaguliwa katika baraza la mawaziri, lakini mwaka 1982, alishtakiwa kwa kosa la kupanga mapinduzi ya kijeshi, baada ya mawakili kutoka Afrika ya Kusini kwenda Zimbabwe central Intelligence Organisation, kujaribu kutengeneza kutokuaminiana kati ya vyama vya ZAPU na chama cha ZANU, waliweka kwa kukusudia silaha katika mashamba yanayomilikwa na chama cha ZAPU na kwenda kutoa taarifa kwa Mugabe juu ya kukutwa kwa silaha katika katika mashamba hayo Katika hotuba yake, Mugabe alisema “ZAPU and its leader Dr. Joshua Nkomo, are like a cobra in a house the only way to deal with effectively with a snake is to strike and destroy its head ” yaani “ZAPU na kiongozi wake, Dr Joshua Nkomo ni kama nyoka ndani ya nyumba, njia pekee ya kufanya kwa nyoka na kumshambulia na kuharibu kichwa chake” Aliagiza kikosi cha jeshi kwa eneo analokaa Nkomo, yaani katika ardhi ya Matebele katika oparesheni ya Gukurahundi na kuua wandebele 3,000 katika jaribio la kutokomeza chama cha ZAPU na kutengeneza serikali chini ya chama kimoja. Nkomo alitoroka Nchini Zimbabwe, na Serkali ya Mugabe ikadai kuwa ametoroka akiwa amevaa kama mwanamke.
NKOMO KATOROKA: Kiongozi wa chama cha ZAPU, emetoroka kwenda katika maficho aliyojipa mwenyewe jijini London baada ya ya kutoroka bila kufuata sheria kupitia Botswana akiwa amevalia kama mwanamke tarehe07/03/1983, akidai kuwa maisha yake yalikuwa hatarini na kuwa alikiwa akienda kutafuta masuluhisho ya Zimbabwe nje ya nchi (chapa ya serikali, Harare 1984) )[4].
Nkomo alidharau madai kuwa, alitoroka akiwa amevalia kama mwanamke, na kusema kuwa "I expected they would invent stupid stories about my flight..... People will believe anything if they believe that ". [4] He added that "...nothing in my life had prepared me for persecution at the hands of a government led by black Africans."[4]
Yaani, “ nilitegemea kuwa wataibua habari za kipumbavu juu ya kuondoka kwangu.,… watu wataamini chochote kama wameamini hayo” na kuongeza kuwa “hakuna kitu katika maisha yangu kilichoandakiwa kwa ajili ya kushtakiwa katika mikono ya serikali ya waafrika weusi. Baada ya amuaji ya kinyama katika Gukurahundi ya mwaka 1987, Nkomo hatimaye akakubali chama cha ZAPU kuingia katika chama cha ZANU, na kusababisha kuotkea kwa chama cha ZANU-PF na kuiacha nchi ya Zimbabwe kama nchi iliyo katika mfumo wa chama kimoja. Jambo lililosababisha baadhi ya watu wa kabila la Ndebele kumlaumu Nkomo kwa kuwauza kwa chama cha kigine. Lakini idadi ya watu wa kabila la Ndebele, walikuwa wachache kiasi cha kushindwa kutoa pingamizi lenye nguvuwakati wa kuunganishwa kwa vyama hivyo viwili. Katika hali ya kutokuwa na nguvu, na afya yake kuzidi kudorora hata ushawishi wake ukashindwa kuwa na mshiko na hivyo kufa Alipoulizwa katika maisha yake, kuwa kwa nini aliruhusu haya yote yatokee, alimwambia mwana historia kuwa Eliaki Sibanda kuwa, alifanya hivyo ili kusitisha mauaji ya watu wa kabila la Ndebele (ambao walikuwa wakiunga mkono chama chake) na ya wanasiasa wa chama cha ZAPU na wanaharakati ambao walikuwa wakilengwa na vyombo vya usalama vya Zimbabwe tangu mwaka 1982, alisema “Mugabe and his Shona henchmen have always sought the extermination of the Ndebele," yaani “Mugabe na Washona wake walitaka kufanya ukatili kwa Wandebele” alisema Nkomo amekuwa si muumini mzuri wa kanisa la kimeshenari katika sehemu kubwa ya maisha yake, alibadilisha dini na kuwa Mkatoliki Roman Catholicism mwaka 1999, muda mfupi baada ya kufariki kwa saratani ya kibofu yaani prostate cancer tarehe 01/07/1999 akiwa na umri wa mika 82, katika hospitali ya Parirenyatwa katika jimbo la Harare

barua za Nkomo

Madai ya kuandikwa kwa barua na Nkomo kwenda kwa waziri mkuu Robert Mugabe akiwa uhamishoni, Uingereza yalianza kuibuka baada ya kifo chake mwaka 1999. katika barua zake , alilalamika kuhusu mateso yake na kuilamu serikali ya Zimbabwe kwa kutokomeza vyama vya upinzani. .[5]

Hadhi ya Kuwa shujaa wa taifa

Mwaka 1999, Nkomo alitangazwa kuwa shujaa, na alizikwa katika makaburi ya mashujaa ya taifa Natioanal Heroes Acre katika jimbo la Harare Tarehe 27/06/2000, seti ya stampu nne zilitolewa na shirika na pasta na mawasiliano la Zimbabwe na kuonesha Joshua Nkomo. Zenye kuonesha badili la fedha ya ZW$2.00, $9.10, $12.00 and $16.00 ya yalikusudiwa na Cedric D Herbert.

Marejeo

  1. Jump up Jessup, John E. An Encyclopedic Dictionary of Conflict and Conflict Resolution, 1945-1996. Page 533.
  2. Jump up Hill, Geoff. The Battle for Zimbabwe: The Final Countdown, 2003. Page 52.
  3. Jump up Cline, Lawrence E. (2005) Pseudo Operations and Counterinsurgency: Lessons from other countries, Strategic Studies Institute, read herep.11
  4. Jump up to: 4.0 4.1 4.2 Joshua Nkomo, The Story of My Life, Methuen London 1984 or Sapes books Harare 2001, p.1-4 "clown Herbert Ushewokunze, minister of home affairs"
  5. Jump up [1] Zimbabwe Metro
  • Nkomo: The Story of My Life, Joshua Nkomo, Nicholas Harman (Author); 1984; ISBN 0413545008,ISBN 978-0413545008, Autobiography
  • The Zimbabwe African People's Union 1961-1987: A Political History of Insurgency in Southern Rhodesia.
  • Terence O. Ranger, ‘Nkomo, Joshua Mqabuko Nyongolo (1917–1999), Oxford Dictionary of National Biography, Oxford University Press, 2004 accessed 18 June 2006

Wednesday 20 November 2013

Mashambulio ya kigaidi ya Afrika ya Mashariki

Mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki

Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi baada ya shambulio, mabaki ya jengo la Ufundi, nyuma kwenye picha Mtaa wa Hailse Selassie na kituo cha reli
Mabaki ya magari yaliyoharibiwa wakati wa mlipuko
Mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki yalitokea katika miji ya Daressalam na Nairobi kwa kulipusha malori yaliyojaa baruti mbele ya balozi za Marekani kila mahali. Angalau watu 224 waliuawa na maelfu kujeruhiwa.
Watendaji walikuwa raia wa nchi za Kenya na Tanzania pamoja na nchi za Kiarabu mbalimbali. Walitekeleza mashambulio kwa maagizo ya kundi la Jihadi ya Kiislamu ya Misri ambalo ni sehemu ya mtandao wa Al Qaida iliyoongozwa na Osama bin Laden.

Shambulio la Nairobi[hariri]

Mnamo saa nne na nusu asubuhi ya siku ya Ijumaa 7 Agosti watu wawili walioendesha lori dogo kilogramu 700 za baruti walifika mbele ya ubalozi wa Marekani iliyokuwepo njiapanda ya barabara za Moi na Haile Selassie karibu na kituo cha reli. Dereva Azzam aliingia kwenye njia ya kutoka katika maegesho ya magari akajaribu kufikia gereji chini ya ubalozi. Hapa alizuiliwa na mlinzi Benson Okuku Bwaku aliyekataa kufungua geti ya gereji. Gaidi wa pili Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali alimtupia kombora ya mkononi lakini alimkosea. Bwaku alifaulu kukimbia na kufikia kona ya jengo akajiokoa. Hapo Azzam alianza kufyatua risasi hovyo. Hapo Al-Owhali alikimbia kuelekea mtaa wa Haile Selassie akajiokoa wakati Azzam akajilipusha kwa baruti kwenye lori. Mlipuko mkubwa ulitikisisha ubalozi na jengo jirani la Ufundi Building. Mshtuko wa mlipuko uliharibu pia vyoo vya madirisha katika kipenyo cha kilomita 1 na sauti yake ilisikika kwa umbali wa kilomita 16.
Jengo la ubalozi liliharibiwa kiasi tu kwa jumla likasimama kwa sababu lilijengwa imara. Ndani ya ubalozi walikufa watu 44, Wamarekani 12 na wafanyakazi wengine 32, wengi wao Wakenya hasa kama waliathiriwa na mshtuko ulioingia madirishani na kuangusha kuta za ndani.
Vifo vingi vilitokea kwa sababu jengo dogo jirani la Ufundi building libomolewa kabisa na kuanguka. Wahanga wengi walikuwa vijana wanafunzi waliosoma kwenye chuo cha ukarani ndani ya jengo hili pamoja na walimu na wafanyakazi wake.
Pamoja na watu waliojeruhiwa katika majengo ya karibu sana kuna wengi waliouawa na kujeruhiwa kwenye barabara ya Haile Selassie kwa sababu moto na mshtuko wa bomu zilielekezwa kati ya kuta za ubalozi na Ufundi Building. Basi iliyokwama kwenye msongamano wa magari mbele ya kiingilio cha ubalozi ilichomwa kabisa pamoja na abiria zake.
Watu wengi walijeruhiwa macho kwa vipande vya kioo; walisikia mlipuko wa kwanza wa kombora la mkononi na risasi zilizofyatuliwa a Azzam wakaenda madirishani kuangalia kuna nini wakapigwa vipande vya kioo cha madirisha usoni wakati bomu ililipuka.

Shambulio la Dar es Salaam[hariri]

Karibu kwenye dakika ya mlipuko wa Nairobi shambulio la pili lilitokea kwenye ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam. Hata hapa dereva alijaribu kuingia kwenye eneo la ubalozi kwa lori lakini alikataliwa getini akalipusha mzigo wake. Hapa ni watu 11 waliokufa na 85 waliojeruhiwa. Idadi ya wahenga ilikuwa ndogo kuliko Nairobi kwa sababu ubalozi ulikuwepo nje ya kitovu cha jiji kando la mtaa wa Bagamoyo na nafasi likuwa kubwa hadi majengo ya jirani.
Mwaka uleule washiriki wa kwanza wa mashambulio haya walikamatwa na kukabidhiwa kwa Marekani. Hadi mwaka 2010 watu 5 walihukumiwa jela ya maisha kwa kushiriki katika ugaidi wa 7 Agosti.

Viungo vya Nje[hariri]

Monday 18 November 2013

Mtakatifu Paulo

Mtakatifu Paulo

Sanamu ya Mtakatifu Paulo mbele yaKanisa kuu la Roma.
Sura yake kadiri ya wataalamu wa LKANorth Rhine-WestphaliaUjerumani.
Mtume Paulo (7-67 hivi) ni mmisionari mkuu wa Yesu Kristo katika historia ya Kanisa.
Alimaliza ushuhuda wake kwa Yesu kwa kufia dini yake mjini Roma chini ya Kaisari Nero.

Maisha kabla ya uongofu[hariri]

Mtakatifu Paulo alizaliwa kati ya miaka 7-10 BK katika familia ya Kiyahudi ya kabila la Benyamini (Israeli) na madhehebu ya Mafarisayo iliyoishi katika mji waTarsus (kwa sasa mji huo uko sehemu ya kusini mashariki ya nchi ya Uturuki).
Jina lake la kwanza (la Kiebrania) lilikuwa Sauli, lakini kadiri ya desturi ya wakati ule alikuwa pia na jina la KigirikiPaulos kutoka Kilatini Paulus (= mdogo). Mwenyewe alikuwa na uraia wa Roma kama wananchi wote wa Tarsus.
Angali kijana alisomea ualimu wa Sheria (yaani wa Torati) huko Yerusalemu chini ya mwalimu maarufu Gamalieli wa madhehebu ya Mafarisayo.
Akishika dini yake kwa msimamo mkali akawa anapinga Ukristo kwa kuwakamata, kuwatesa na hata kuwaua Wakristo, kama vile Stefano Mfiadini mpaka alipotokewa na Yesu Kristo mfufuka akiwa njiani kwenda Damaski (kwa umuhimu wake katika Historia ya Wokovu habari hii inasimuliwa mara tatu katika kitabu chaMatendo ya Mitume: 9:1-19; 21:12-18 na 22:5-16). Jibu lake kwa Yesu lilikuwa (Mdo 22:10): "Nifanye nini, Bwana?"

Baada ya uongofu[hariri]

Baada ya kufanya utume katika mazingira ya Kiarabu, Tarsus na Antiokia alianza kufanya safari za kitume, akienda mbali zaidi na zaidi, akilenga kumhubiri Yesumahali ambapo bado hajafahamika, hata Hispania.
Ilikuwa kawaida yaKE kuanzisha Kanisa katika miji mikubwa ili toka huko ujumbe ufike hadi vijijini.
Muda wote wa utume wake Paulo alipambana na dhuluma kutoka kwa Wayahudi wenzake na matatizo mengine kutoka Wakristo wenye msimamo tofauti na wa kwake hasa kuhusu haja ya kufuata masharti ya Agano la Kale ili kupata wokovu.
Hatimaye alikamatwa na wapinzani wake Wayahudi mjini Yerusalemu, lakini askari wakoloni walizuia asiuawe.
Baada ya hapo alilazimika kukaa gerezani akisubiri hukumu ya Dola la Roma, kwanza Kaisaria Baharini miaka miwili, halafu akakata rufaa kwa Kaisari akapelekwa Roma, alipofika mwaka 61 akakaa miaka miwili tena kifungo cha nje katika nyumba ya kupanga.
Kisha kufunguliwa (labda kwa sababu washtaki wake hawakuwasili) alisafiri tena ingawa hakuna hakika alielekea wapi.

Kifodini chake[hariri]

Aliuawa nje ya kuta za Roma kwa kukatwa kichwa wakati wa dhuluma za Nero kati ya mwaka 64 na 67 B.K.
Juu ya kaburi lake lilijengwa kanisa kubwa ambalo liliteketea kwa moto katika karne ya 18 likajengwa upya na hadi leo linapokea hija za Wakristo wengi, hasa katika Jubilei ya mtume Paulo iliyotangazwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kwa mwaka 2008/2009.

Maandishi yake[hariri]

Agano Jipya

Kati ya barua nyingi alizoandikwa kwa makanisa ya ThesalonikeKorinthoGalatia, Roma, FilipiKolosaiEfeso, kwa viongozi Wakristo kama Timotheo na Tito, tena kwa Filemoni, katika Agano Jipya zinatunzwa 13.
Ukubwa na ubora wa mchango wa Paulo unaeleweka tukizingatia kwamba alifanya kazi na kuandika kabla ya vitabu vya Agano Jipya kupatikana. Ndiye aliyeanza kuliandika akipanua mawazo aliyoyapokea katika Kanisa kwa kuzingatia Agano la Kale na mang’amuzi yake mwenyewe.
Hapo alifafanua vizuri ajabu maisha ya Kikristo kama neema ya kumshiriki Yesu kwa imanisakramenti na juhudi za kushinda umimi hadi kugeuka sadaka hai, takatifu na ya kumpendeza Mungu.
Wokovu huo, utakaokamilika katika ufufuko wa mwili, unapatikana katika Kanisa, ambalo Paulo alilitambulisha kama bibiarusi wa Kristo na mwili wake.

Marejeo[hariri]

  • Aulén, GustafChristus Victor (SPCK 1931)
  • Brown, Raymond E. An Introduction to the New Testament. Anchor Bible Series, 1997. ISBN 0-385-24767-2.
  • Brown, Raymond E. The Church the Apostles left behind(Chapman 1984)
  • Bruce, F.F. 'Is the Paul of Acts the Real Paul?' Bulletin John Rylands Library 58 (1976) 283–305
  • Bruce, F.F.Paul: Apostle of the Heart Set Free (ISBN 0-8028-4778-1)
  • Conzelmann, Hansthe Acts of the Apostles—a Commentary on the Acts of the Apostles (Augsburg Fortress 1987)
  • Davies, W. D. "The Apostolic Age and the Life of Paul" in Matthew Black, ed. Peake's Commentary on the Bible. London: T. Nelson, 1962. ISBN 0-8407-5019-6
  • Davies, W. D. Paul and Rabbinic Judaism: Some Rabbinic Elements in Pauline Theology. S.P.C.K., 3rd ed., 1970. ISBN 0-281-02449-9
  • Dunn, James D.G., 1990, Jesus, Paul and the Law Louisville,KY: Westminster John Knox Press. ISBN 0-664-25095-5
  • Dunn, James D. G., Jesus, Paul, and the Gospels (Grand Rapids (MI), Wm. B. Eerdmans, 2011).
  • Hanson, Anthony T. Studies in Paul's Technique and Theology. Eerdmans, 1974. ISBN 0-8028-3452-3
  • Harris, Stephen L. Understanding the Bible. Palo Alto: Mayfield. 1985. ISBN 978-1-55934-655-9
  • Holzbach, Mathis Christian, Die textpragmat. Bedeutung d. Kündereinsetzungen d. Simon Petrus u.d. Saulus Paulus im lukan. Doppelwerk, in: Jesus als Bote d. Heils. Stuttgart 2008, 166-172.
  • IrenaeusAgainst Heresies, i.26.2
  • Maccoby, HyamThe Mythmaker: Paul and the Invention of Christianity. New York: Harper & Row, 1986. ISBN 0-06-015582-5.
  • Kim, Yung Suk. A Theological Introduction to Paul's Letters. Eugene, Oregon: Cascade Books, 2011. ISBN 978-1-60899-793-0
  • MacDonald, Dennis Ronald, 1983. The Legend and the Apostle: The Battle for Paul in Story and Canon Philadelphia: Westminster Press.
  • Murphy-O'Connor, Jerome, Jesus and Paul: Parallel lives (Collegeville, Minn.: Liturgical Press, 2007) ISBN 0-8146-5173-9
  • Murphy-O'Connor, Jerome, Paul the Letter-Writer: His World, His Options, His Skills (Collegeville, Minn.: Liturgical Press, 1995) ISBN 0-8146-5845-8
  • Murphy-O'Connor, Jerome, Paul: A Critical Life (Oxford: Clarendon Press, 1996) ISBN 0-19-826749-5
  • Ogg, George. “Chronology of the New Testament.” Matthew Black, ed. ‘’Peake's Commentary on the Bible.’’ Nelson, 1962. ISBN 0-8407-5019-6
  • Rashdall, Hastings, The Idea of Atonement in Christian Theology (1919)
  • Ruef, John, Paul's First letter to Corinth (Penguin 1971)
  • Sanders, E.P.Paul and Palestinian Judaism (1977)
  • Segal, Alan F. Paul, the Convert, (New Haven/London, Yale University Press, 1990) ISBN 0-300-04527-1.
  • Segal, Alan F., "Paul, the Convert and Apostle" in Rebecca's Children: Judaism and Christianity in the Roman World (Harvard University Press 1986).
  • Horrell, David G. "An Introduction to the Study of Paul." T&T Clark Approaches to Biblical Studies. 2nd edition. London: T&T Clark, 2006

Marejeo mengine[hariri]

  • Bart D Ehrman. Peter, Paul and Mary Magdalene: The Followers of Jesus in History and Legend; 304 pages, Oxford University Press (Machi 2008)
  • Bart D. Ehrman. The New Testament: A Historical Introduction to the Early Christian Writings; 608 pages, Oxford University Press (Julai 2011); ISBN 978-0-19-975753-4
  • Hyam MacCoby. The Mythmaker: Paul and the Invention of Christianity; 238 pages, Barnes & Noble Books (1998); ISBN 978-0-7607-0787-6
  • Hans Joachim Schoeps. Paul: The Theology of the Apostle in the Light of Jewish Religious History (Library of Theological Translations); 34 pages, Lutterworth Press (Julai 2002); ISBN 978-0-227-17013-7
  • Pinchas Lapide, Peter Stuhlmacher. Paul: Rabbi and Apostle; 77 pages, Augsburg Publishing House; (Desemba 1984)
  • Pinchas Lapide, Leonard Swidler, Jurgen Moltmann. Jewish Monotheism and Christian Trinitarian Doctrine; 94 pages, Wipf & Stock Publishers (Mei 2002)

Viungo vya nje[hariri]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: