member

Thursday 24 October 2013

vita vya pili vya dunia


Vita Kuu ya Pili ya Dunia Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa vita kuanzia 1939 hadi 1945 ya Ujerumani, Italia, Japani na mataifa yaliyoshikamana nao (Romania, Hungaria na Bulgaria) dhidi ya nchi nyingi za dunia (ziliitwa mataifa ya ushirikiano) kati yao hasa Uingereza, Ufaransa, Urusi na Marekani. Yaliyomo [ficha] 1 Vita Kuu ya Dunia 2 Mwanzo wa vita 3 Vita katika Ulaya 4 Vita ya kidunia 5 Mwisho wa vita 6 Wafu wa vita 7 Umoja wa Mataifa Vita Kuu ya Dunia[hariri] Jina limepatikana kutokana na vita ya miaka 1914 - 1918 iliyoona mapambano kati ya Ujerumani na wenzake dhidi ya nchi nyingi. Vita ya 1914/1918 iliitwa "Vita Kuu ya Dunia" kwa sababu mapigano yalienea pande nyingi za dunia yote tofauti na vita zilizotangulia. Kwa namna fulani vita iliyoanza 1939 ilikuwa marudio ya vita iliyotangulia. Hivyo imekuwa kawaida kuzitaja vita hizi kama Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili ya Dunia. Mwanzo wa vita[hariri] Vita hii ilianza huko Ulaya tar. 1 Septemba 1939 kwa mashambulizi ya Wajerumani dhidi Poland. Wengine huhesabu mashambulizi ya Japani dhidi Uchina tar. 07.07. 1937 kuwa mwanzo wa vita. Mwisho wake ulikuwa huko Ulaya tar. 9 Mei 1945 halafu huko Asia tar. 2 Septemba 1945. Vita katika Ulaya[hariri] Mashambulizi ya Wajerumani dhidi Poland ilisababisha hali ya vita kati ya Ujerumani kwa upande moja na Ufaransa na Uingereza kwa upande mwingine waliokuwa na mkataba ya kulindana na Poland. Serikali za Australia, New Zealand, Nepal, Afrika Kusini na Kanada zilishikamana na Uingereza kwa kutangaza vita dhidi Ujerumani. Urusi ulikuwa na mkataba wa siri na Ujerumani ulichukua nafasi ya kuteka sehemu kubwa za Poland ya Mashariki. Mwezi wa Aprili 1940 Waingereza walianza kupeleka wanajeshi Norway wakiwa na shabaha ya kuzuia kupelekwa kwa madini ya chuma kutoka Sweden kwenda Ujerumani kupitia mabandari ya Norway. Wajerumani walichukua nafasi hii kuteka Denmark na Norway na kufukuza Waingereza. Mei 1940 Wajerumani walishambulia Ufaransa pamoja na nchi za Uholanzi, Ubelgiji na Luxemburg. Vita hii ilikwisha haraka Wajerumani walishinda na kupiga pia kikosi cha Waingereza huko Ufaransa. Baadaye walisitasita kushambulia Uingereza peyewe. Mipango yao ilihitaji mbinu za kuvuka bahari. Wakajaribu kuvuruga nguvu ya kijeshi ya Waingereza kwa mashambulizi ya ndege lakini hawakuwa na uwezo wa kutosha. Katika shambulizi dhidi ya Ufaransa Waitalia walishirikiana kwa upande wa Wajerumani. Mwisho wa 1940 Waitalia walianza kuwashambulia Ugiriki na jeshi la Waingereza huko Misri na Malta. Lakini mahali pote walirudishwa nyuma hadi kiongozi Mjerumani Adolf Hitler aliamua kuwasaidia Waitalia na kupeleka wanajeshi Wajerumani kwenda Afrika ya Kaskazini pamoja na Ugiriki mwaka 1941. Hii ilisababisha pia Wajerumani kuteka Yugoslavia wakiwa njiani kwenda Ugiriki. Vita ya kidunia[hariri] Mwaka wa 1941 uliona vita kubadilika kutoka vita ya Kiulaya kuwa vita ya kidunia. 'Wajerumani walishambulia Urusi' wakifika hadi kando la mji mkuu wa Moscow lakini walishindwa kuiteka. Walikamata kusini yote ya Urusi hadi milima ya Kaukazi na hadi mto wa Wolga. Wajapani walishambulia Marekani' pamoja na makoloni ya Waingereza na Waholanzi huko Asia. Hitler alitangaza pia vita dhidi ya Marekani akitaka kuwasaidia Wajapan ingawa Japan haikushambulia Urusi. Katika miaka iliyofuata nguvu ya Ujerumani na Japani ilipungua. Hasa uwezo wa kiuchumi wa Marekani ulizalisha mitambo na silaha kwa mkasi usiopatikana kwa Wajerumani na Wajapon. Ukali wa utetezi wa Warusi ulichosha nguvu za Wajerumani. Kuanzia mwaka 1943 mataifa ya ushirikiano yalianza kusogea mbele pande zote. Warusi walisukuma Wajerumani polepole warudi nyuma. Waamerika na Waingereza walipeleka wanajeshi Italia ya Kusini. Italia iliona mapinduzi kiongozi Mwitalia Mussolini aliondolewa madarakani na serikali mpya ilijiunga na mataifa ya ushirikiano. 1944 mataifa ya ushirikiano waliingia Ufaransa wakielekea Ujerumani. Wakati huohuo Warusi walisogea mbele zaidi wakikaribia mipaka ya Ujerumani. Huko Asia Japon ilipotea sehemu kubwa sana ya meli zake za kivita na Jeshi la Marekani lilikaribia visiwa vya Japani tayari. Mwisho wa vita[hariri] 1945 iliona mwisho wa vita. Mataifa mengi yaliyokuwa mbali kama Argentina, Peru au Mongolia yalitangaza pia hali ya vita dhidi Ujerumani na Japani. Pia nchi zilizowahi kushikamana na Wajerumani waligeukia mataifa ya ushirikoano. Ujerumani penyewe ilivamiwa kutoka Magharibi na Mashariki. Warusi walifika mji mkuu wa Berlin na Adolf Hitler alijiua tar. 30 Aprili 1945; wanajeshi wake walitia sahihi mkataba wa kusalimu amri tar. 08./09. 05. 1945. Wingu la kinyuklia juu ya Nagasaki tar. 9.8.1945 Huko Asia Japani iliendelea kupigana na Waamerika walioweza kufikisha ndege zao zilizobeba mabomu hadi Japoni penyewe. Agosti 1945 Waamerika walitumia silaha mbili za kinyuklia walizokuwa nazo wakati ule na kuua watu wengi sana huko Hiroshima tar. 6 Agosti na Nagasaki tar. 9 Agosti 1945. Siku zilezile Warusi walianza kuwashambulia wanajeshi Wajapani huko Uchina. Haya yote yalisababisha serikali ya Japani kukubali wameshindwa wakatia sahihi mkataba wa kusalimu amri tar. 02.09.1945. Wafu wa vita[hariri] Kwa jumla takriban watu millioni 60 walikufa kutokana na vita hivi. Makadirio hutaja wanajeshi millioni 25 na watu raia millioni 35. Taifa lililopotea watu wengi ni Urusi walipokufa kati ya millioni 20 - 28, idadi kubwa watu raia. Takriban watu millioni 10 waliuawa na Wajerumani au walikufa kutokana na kutendewa vibaya nje ya mapigano kama vile millioni 6 za Wayahudi, wengine Wapoland, Warusi, Wasinti, walemavu n.k.. Umoja wa Mataifa[hariri] Tokeo moja la vita kuu ya pili ni kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. Uliundwa 1945 kama chombo cha kuzuia vita zijazo. Kutokana na historia hii mataifa yenye nafasi za kudumu na kura ya veto katika Baraza ya Usalama ndiyo mataifa washindi wa vita kuu ya pili: Marekani, Uchina, Ufaransa, Uingereza na Urusi. Kutokana na kura ya veto hawawezi kuondolewa bila kukubali wenyewe hata kama siku hizi Ufaransa na Uingereza si nchi muhimu sana tena duniani.

Friday 18 October 2013

HISTORIA YA HIPHOP

Muziki wa hip hop

Muziki wa hip hop ni aina ya muziki ulioanza kunako miaka ya 1970, ukiwa umeanzishwa na Wamarekani weusi katika miji mikubwa ya Marekani. Hip hop mara nyingi inatumia staili moja ya kuimbaiitwayo kurap au kufokafoka.
Kurap ni staili ya uimbaji ambayo mwimbaji anatoa au anaimba maneno-mashairi yaambatanayo na vina. Mashairi mengi yaliyoimbwa katika muziki wa hip hop yalikuwa yakizungumzia maisha halisi ya watu weusi wa nchini Marekani, sanasana katika miji mikubwa.
Kuna baadhi ya mashairi ya muziki wa hip hop yanazungumzia wahuni, uharifu, na utumiaji haramu wa madawa ya kulevya. Muziki wa hip hop pia huchukua tabia (mwenendo) wa staili za muziki wa pop, yaani kama disko na reggae.

Soma zaidi[hariri]

  • David Toop (1984/1991). Rap Attack II: African Rap To Global Hip Hop. New York. New York: Serpent's Tail. ISBN 1-85242-243-2.
  • McLeod, Kembrew. Interview with Chuck D and Hank Shocklee. 2002. Stay Free Magazine.
  • Yes Yes Y'All: Oral History of Hip Hop's First Decade. Fricke, Jim and Charlie Ahearn (eds). Experience Music Project. Perseus Books Group. ISBN 0-306-81184-7
  • Corvino, Daniel and Livernoche, Shawn (2000). A Brief History of Rhyme and Bass: Growing Up With Hip Hop. Tinicum, PA: Xlibris Corporation/The Lightning Source, Inc. ISBN 1-4010-2851-9
  • Chang, Jeff. "Can't Stop, Won't Stop".
  • Rose, Tricia (1994). "Black Noise". Middletown, Connecticut: Wesleyan University Press. ISBN 0-8195-6275-0
  • Potter, Russell (1995) Spectacular Vernaculars: Hip-Hop and the Politics of Postmodernism. Albany: SUNY Press. ISBN 0-7914-2626-2
  • Light, Alan (ed). (1999). The VIBE History of Hip-Hop. New York: Three Rivers Press. ISBN 0-609-80503-7
  • George, Nelson (2000, rev. 2005). Hip-Hop America. New York: Penguin Books. ISBN 0-14-028022-7
  • Fricke, Jim and Ahearn, Charlie (eds). (2002). Yes Yes Y'All: The Experience Music Project Oral History of Hip Hop's First Decade. New York: Da Capo Press. ISBN 0-306-81184-7
  • Kitwana, Bakar (2004). The State of Hip-Hop Generation: how hip-hop's culture movement is evolving into political power. Retrieved 4 Desemba 2006. From Ohio Link Database.

Tazama pia[hariri]

Viungo vya nje[hariri]