member

Sunday 15 December 2013

HISTORIA YA George Washington

George Washington

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Washington akisimamia shamba na watumwa.
Washington akivuka mto Delaware katika vita ya uhuru ya Marekani.
Sanamu ya Washington pamoja na maraisi wengine kwenye mlima Rushmore
Nyumba yake kwenye shamba la Mount Vernon
Washington kwenye pesa la Marekani.
George Washington (22 Februari 1732 hadi 14 Desemba 1799) alikuwa mwanasiasa, kiongozi wa kijeshi na rais wa kwanza wa Marekani kati ya 1789 na 1797.

Mtoto na kijana[hariri]

Alizaliwa kama mtoto wa pili wa mlowezi Augustine Washington katika koloni ya Virginia iliyokuwa mali ya mfalme wa Uingereza. Wazazi walikuwa na shamba kubwa lililolimwa na watumwa Waafrika. George alisoma shule miaka michache hakuendelea sana kielimu. Baada ya shule alianza kazi ya upimaji na ramani.

Mkulima na kiongozi wa kijeshi[hariri]

Baada ya kifo cha kakaye alirithi shamba kubwa pamoja na watumwa akawa mkulima mtajiri. Sehemu ya urithi ilikuwa cheo cha msimazi wa wanamgambo waliokuwa kikosi cha kijeshi cha hiari waliotakiwa kusaidiana na wanajeshi Waingereza kutetea koloni dhidi ya majirani Waindio na Wafaransa walioenea kuelekea kusini kutoka koloni yao ya Kanada - Quebec.
Katika umri mdogo wa miaka 22 Washington alijikuta kama mkuu wa wanamgambo katika vita ya Uingereza dhidi ya Wafaransa na Waindio iliyopanuka baada ye kuwa Vita ya Miaka Saba. Akaongoza kikosi chake dhidi ya maadui akafaulu mara kadhaa. Baadaye alishirikiana na jeshi rasmi la Uingereza katika mapigano ya Monongahela na kuongoza mabaki ya jeshi baada ya kifo cha jemadari Mwingereza. 1755 akawa mkuu wa jeshi la koloni Virginia. Lakini baada ya ushindi Waingereza walikataa kumpa cheo katika jeshi la mfalme hivyo akajiuzulu akirudi kwa shamba lake na kufuata siasa kwenye bunge la koloni.
1759 Washington akamwoa mjane mtajiri akawa kati ya matajiri kabisa wa Virginia.

Mapinduzi[hariri]

Baada ya vita ya miaka saba uhusiano kati ya Uingereza na walowezi Waingereza katika koloni zake 13 za Amerika ya Kaskazini ukazorota. Tangu 1773 Waingereza walitumia sheria ya dharura na nguvu ya kijeshi mjini Boston. Wawakilishi wa koloni zote 13 wakakutana kama bunge la Amerika Bara na Washington alikuwa miongoni mwao.
Baada ya mapigano ya kwanza kati ya wanajeshi Waingereza na wanamgambo wa walowezi bunge likaamua kuunda jeshi la pamoja la koloni zote na Washington akateuliwa kuwa jemadari mkuu.
Aliongoza jeshi la Marekani katika vita ya uhuru wa Marekani dhidi ya Uingereza hadi mwaka 1783.

Baada ya vita: mwanasiasa na rais[hariri]

Baada ya vita ya uhuru ya Marekani Geroge Washington akarudi kwake akalima tena lakini akachaguliwa pia kama mwakilishi wa Virginia katika bunge la katiba la Marekani mwaka 1787 akawa mwenyekiti wa mkutano huu uliokubali katiba ya Marekani.
4 Februari 1789 alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani akirudishwa mwaka 1789. Baada ya kipindi chake cha pili alikataa kusimama tena akaunda hivyo utaratibu ya kwamba rais anaweza kurudishwa mara moja tu hawezi kuendelea zaidi.

Uzee[hariri]

1797 akarudi tena kwake shambani aliposimamia kilimo kilichoendeshwa na watumwa 390. Tar. 14 Desemba alikufa kwake nyumbani. Kabla ya kuaga dunia aliamuru katika usia wake ya kwamba watumwa wake wote warudishiwe uhuru baada ya kifo chake yeye mwenyewe na mke wake.
Mji mkuu wa Marekani Washington, D.C. na jimbo la Washington vimepokwa majina kutokana naye. Picha yake iko kwenye noti ya dollar moja.

No comments: