member

Saturday 21 December 2013

P FUNK

P. Funk

Paul Majani
P Funk Majani.jpg
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwaPaul Matthysse
Pia anajulikana kamaP Funk, Majani, Kinywele Kimoja, Mdachi nk.
Asili yakeTanzania
Aina ya muzikiHip Hop na Bongo Flava
Kazi yakeMtayarishaji
AlaKinanda,Guitar, Kinakilishi
Miaka ya kazimn. 1995 -
StudioBongo Records
Ame/Wameshirikiana naMaster JayBonny Luv,Rajabu Marijani,Bizz Man, Boznia nk.
Paul Matthysse ( P Funk ) ni mtayarishaji wa muziki na pia mmiliki wa Studio ya Bongo Records iliyopo jijini Dar es SalaamTanzania. P Funk ambaye nusu Mtanzania nusu Mdachi, kama miaka ishirini iliyo pita hivi .P Funk a.k.a Majani, alikuwa na hisia za kupendelea muziki na pindi hadi kuamua kufanya kweli.. kuvutiwa kwake kupenda muziki ndio chanzo kikumbwa.. kilicho pelekea kufanikiwa vizuri katika muziki.
Kwenye Miaka 1991-92 wakati yupo bado shule IST (International School Of Tanganyika. Alikuwa mtundu mtundu kwenye studio za pale shule.. kupiga- piga midundo mbali mbali ya hapa na pale na kufoka-foka(Rap music) na pia alikuwa mbele sana kwa kupiga musiki kwenye Pati mbali mbali.. na hapo alikuwa kupenda sana musiki kwa ujumla.

Elimu ya Muziki na Uzoefu Wake[hariri]

P-Funk alikwenda kimasomo ya Mlio (sound) engineering kwa miezi 18 pale AmsterdamNetherland kabla ajaingia kwenye kutayarisha muziki. Alikuwa anajua kitu anachotaka kufanya. Mwaka 1995 akiwa na vifaa vyake vichache alianzisha kampuni yake ya kurekodi muziki nyumbani kwake. Na ni katika kipindi hicho hicho neno ’Bongo’lilipokuwa linatawala katika misemo ya kiswahili cha mitaani na lilikuwa linaelezea hali halisi ya maisha ya Dar es Salaam na ndio kipindi hicho album ya Bongo ilipozinduliwa. Akiwa bado ni mtayarishaji muziki mdogo, amefanikiwa kupata umaarufu mkubwa katika fani ya muziki na hasa katika milipuko ya nyimbo zenye ladha ya Bongo.
Anakubali kuwa amepata sana utaalam na mbinu kutokana na kufanya kazi watayarishaji wengine wa muziki wa Kitanzania kama Master J, Bonny Love na Rico. Mawazo yake na namna ya kuyaoainisha na muziki ndio hasa ambacho kinafanya muziki wake ufanikiwe.

Tuzo Alizopata[hariri]

Wasanii Aliowainua[hariri]

Kwanza alianza kwa kumpandisha chati Juma Nature ambaye ndio nyota wa nyimbo za Bongo Flava na akaendelea kwa kutayarisha santuri yaSolo ThangAYZay BSista PMike T na pia alishawahi kufanya kazi na Professor Jay alipotoa santuri yake mwenyewe. P Funk ana wasanii wengine wengi wanaotumia nembo ya kampuni yake katika Utengenezaji wa albamu.

Pia Anajulikana Kama[hariri]

  • P Funk
  • Halfani
  • Majani
  • Kinywele Kimoja
  • Mkono wa mungu
Musical notes.svgMakala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu P. Funk kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
safi sana

No comments: