member

Monday 18 November 2013

Mtakatifu Paulo

Mtakatifu Paulo

Sanamu ya Mtakatifu Paulo mbele yaKanisa kuu la Roma.
Sura yake kadiri ya wataalamu wa LKANorth Rhine-WestphaliaUjerumani.
Mtume Paulo (7-67 hivi) ni mmisionari mkuu wa Yesu Kristo katika historia ya Kanisa.
Alimaliza ushuhuda wake kwa Yesu kwa kufia dini yake mjini Roma chini ya Kaisari Nero.

Maisha kabla ya uongofu[hariri]

Mtakatifu Paulo alizaliwa kati ya miaka 7-10 BK katika familia ya Kiyahudi ya kabila la Benyamini (Israeli) na madhehebu ya Mafarisayo iliyoishi katika mji waTarsus (kwa sasa mji huo uko sehemu ya kusini mashariki ya nchi ya Uturuki).
Jina lake la kwanza (la Kiebrania) lilikuwa Sauli, lakini kadiri ya desturi ya wakati ule alikuwa pia na jina la KigirikiPaulos kutoka Kilatini Paulus (= mdogo). Mwenyewe alikuwa na uraia wa Roma kama wananchi wote wa Tarsus.
Angali kijana alisomea ualimu wa Sheria (yaani wa Torati) huko Yerusalemu chini ya mwalimu maarufu Gamalieli wa madhehebu ya Mafarisayo.
Akishika dini yake kwa msimamo mkali akawa anapinga Ukristo kwa kuwakamata, kuwatesa na hata kuwaua Wakristo, kama vile Stefano Mfiadini mpaka alipotokewa na Yesu Kristo mfufuka akiwa njiani kwenda Damaski (kwa umuhimu wake katika Historia ya Wokovu habari hii inasimuliwa mara tatu katika kitabu chaMatendo ya Mitume: 9:1-19; 21:12-18 na 22:5-16). Jibu lake kwa Yesu lilikuwa (Mdo 22:10): "Nifanye nini, Bwana?"

Baada ya uongofu[hariri]

Baada ya kufanya utume katika mazingira ya Kiarabu, Tarsus na Antiokia alianza kufanya safari za kitume, akienda mbali zaidi na zaidi, akilenga kumhubiri Yesumahali ambapo bado hajafahamika, hata Hispania.
Ilikuwa kawaida yaKE kuanzisha Kanisa katika miji mikubwa ili toka huko ujumbe ufike hadi vijijini.
Muda wote wa utume wake Paulo alipambana na dhuluma kutoka kwa Wayahudi wenzake na matatizo mengine kutoka Wakristo wenye msimamo tofauti na wa kwake hasa kuhusu haja ya kufuata masharti ya Agano la Kale ili kupata wokovu.
Hatimaye alikamatwa na wapinzani wake Wayahudi mjini Yerusalemu, lakini askari wakoloni walizuia asiuawe.
Baada ya hapo alilazimika kukaa gerezani akisubiri hukumu ya Dola la Roma, kwanza Kaisaria Baharini miaka miwili, halafu akakata rufaa kwa Kaisari akapelekwa Roma, alipofika mwaka 61 akakaa miaka miwili tena kifungo cha nje katika nyumba ya kupanga.
Kisha kufunguliwa (labda kwa sababu washtaki wake hawakuwasili) alisafiri tena ingawa hakuna hakika alielekea wapi.

Kifodini chake[hariri]

Aliuawa nje ya kuta za Roma kwa kukatwa kichwa wakati wa dhuluma za Nero kati ya mwaka 64 na 67 B.K.
Juu ya kaburi lake lilijengwa kanisa kubwa ambalo liliteketea kwa moto katika karne ya 18 likajengwa upya na hadi leo linapokea hija za Wakristo wengi, hasa katika Jubilei ya mtume Paulo iliyotangazwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kwa mwaka 2008/2009.

Maandishi yake[hariri]

Agano Jipya

Kati ya barua nyingi alizoandikwa kwa makanisa ya ThesalonikeKorinthoGalatia, Roma, FilipiKolosaiEfeso, kwa viongozi Wakristo kama Timotheo na Tito, tena kwa Filemoni, katika Agano Jipya zinatunzwa 13.
Ukubwa na ubora wa mchango wa Paulo unaeleweka tukizingatia kwamba alifanya kazi na kuandika kabla ya vitabu vya Agano Jipya kupatikana. Ndiye aliyeanza kuliandika akipanua mawazo aliyoyapokea katika Kanisa kwa kuzingatia Agano la Kale na mang’amuzi yake mwenyewe.
Hapo alifafanua vizuri ajabu maisha ya Kikristo kama neema ya kumshiriki Yesu kwa imanisakramenti na juhudi za kushinda umimi hadi kugeuka sadaka hai, takatifu na ya kumpendeza Mungu.
Wokovu huo, utakaokamilika katika ufufuko wa mwili, unapatikana katika Kanisa, ambalo Paulo alilitambulisha kama bibiarusi wa Kristo na mwili wake.

Marejeo[hariri]

  • Aulén, GustafChristus Victor (SPCK 1931)
  • Brown, Raymond E. An Introduction to the New Testament. Anchor Bible Series, 1997. ISBN 0-385-24767-2.
  • Brown, Raymond E. The Church the Apostles left behind(Chapman 1984)
  • Bruce, F.F. 'Is the Paul of Acts the Real Paul?' Bulletin John Rylands Library 58 (1976) 283–305
  • Bruce, F.F.Paul: Apostle of the Heart Set Free (ISBN 0-8028-4778-1)
  • Conzelmann, Hansthe Acts of the Apostles—a Commentary on the Acts of the Apostles (Augsburg Fortress 1987)
  • Davies, W. D. "The Apostolic Age and the Life of Paul" in Matthew Black, ed. Peake's Commentary on the Bible. London: T. Nelson, 1962. ISBN 0-8407-5019-6
  • Davies, W. D. Paul and Rabbinic Judaism: Some Rabbinic Elements in Pauline Theology. S.P.C.K., 3rd ed., 1970. ISBN 0-281-02449-9
  • Dunn, James D.G., 1990, Jesus, Paul and the Law Louisville,KY: Westminster John Knox Press. ISBN 0-664-25095-5
  • Dunn, James D. G., Jesus, Paul, and the Gospels (Grand Rapids (MI), Wm. B. Eerdmans, 2011).
  • Hanson, Anthony T. Studies in Paul's Technique and Theology. Eerdmans, 1974. ISBN 0-8028-3452-3
  • Harris, Stephen L. Understanding the Bible. Palo Alto: Mayfield. 1985. ISBN 978-1-55934-655-9
  • Holzbach, Mathis Christian, Die textpragmat. Bedeutung d. Kündereinsetzungen d. Simon Petrus u.d. Saulus Paulus im lukan. Doppelwerk, in: Jesus als Bote d. Heils. Stuttgart 2008, 166-172.
  • IrenaeusAgainst Heresies, i.26.2
  • Maccoby, HyamThe Mythmaker: Paul and the Invention of Christianity. New York: Harper & Row, 1986. ISBN 0-06-015582-5.
  • Kim, Yung Suk. A Theological Introduction to Paul's Letters. Eugene, Oregon: Cascade Books, 2011. ISBN 978-1-60899-793-0
  • MacDonald, Dennis Ronald, 1983. The Legend and the Apostle: The Battle for Paul in Story and Canon Philadelphia: Westminster Press.
  • Murphy-O'Connor, Jerome, Jesus and Paul: Parallel lives (Collegeville, Minn.: Liturgical Press, 2007) ISBN 0-8146-5173-9
  • Murphy-O'Connor, Jerome, Paul the Letter-Writer: His World, His Options, His Skills (Collegeville, Minn.: Liturgical Press, 1995) ISBN 0-8146-5845-8
  • Murphy-O'Connor, Jerome, Paul: A Critical Life (Oxford: Clarendon Press, 1996) ISBN 0-19-826749-5
  • Ogg, George. “Chronology of the New Testament.” Matthew Black, ed. ‘’Peake's Commentary on the Bible.’’ Nelson, 1962. ISBN 0-8407-5019-6
  • Rashdall, Hastings, The Idea of Atonement in Christian Theology (1919)
  • Ruef, John, Paul's First letter to Corinth (Penguin 1971)
  • Sanders, E.P.Paul and Palestinian Judaism (1977)
  • Segal, Alan F. Paul, the Convert, (New Haven/London, Yale University Press, 1990) ISBN 0-300-04527-1.
  • Segal, Alan F., "Paul, the Convert and Apostle" in Rebecca's Children: Judaism and Christianity in the Roman World (Harvard University Press 1986).
  • Horrell, David G. "An Introduction to the Study of Paul." T&T Clark Approaches to Biblical Studies. 2nd edition. London: T&T Clark, 2006

Marejeo mengine[hariri]

  • Bart D Ehrman. Peter, Paul and Mary Magdalene: The Followers of Jesus in History and Legend; 304 pages, Oxford University Press (Machi 2008)
  • Bart D. Ehrman. The New Testament: A Historical Introduction to the Early Christian Writings; 608 pages, Oxford University Press (Julai 2011); ISBN 978-0-19-975753-4
  • Hyam MacCoby. The Mythmaker: Paul and the Invention of Christianity; 238 pages, Barnes & Noble Books (1998); ISBN 978-0-7607-0787-6
  • Hans Joachim Schoeps. Paul: The Theology of the Apostle in the Light of Jewish Religious History (Library of Theological Translations); 34 pages, Lutterworth Press (Julai 2002); ISBN 978-0-227-17013-7
  • Pinchas Lapide, Peter Stuhlmacher. Paul: Rabbi and Apostle; 77 pages, Augsburg Publishing House; (Desemba 1984)
  • Pinchas Lapide, Leonard Swidler, Jurgen Moltmann. Jewish Monotheism and Christian Trinitarian Doctrine; 94 pages, Wipf & Stock Publishers (Mei 2002)

Viungo vya nje[hariri]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

No comments: