member

Friday 8 November 2013

Steven Kanumba

Steven Kanumba

Steven Kanumba
Steven-Kanumba.jpg
Hayati Steven Kanumba.
AmezaliwaSteven Charles Kanumba
Januari 8 1984 (umri 29)ShinyangaTanzania
AmekufaAprili 7, 2012 (umri 28) Dar es SalaamTanzania
Kazi yakeMuigizajiMtunziMtayarishaji,Muongozaji
Steven Charles Kanumba (8 Januari 1984Shinyanga - 7 Aprili 2012) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka nchini Tanzania. Katika historia ya tasnia ya filamu nchini Tanzania, Kanumba ndiye aliyekuwa msanii wa kwanza nchini kufanya kazi nje ya nchi na kuweza kuwavuta wageni kutoka nchi mbalimbali kuja kuigiza Tanzania. Hasa walikuwa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah, na wengine wengi tu. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa was Kinigeria nchini.

Maisha

Steven alianza masomo yake katika shule ya msingi yaBugoyi, na kuendela na masomo ya sekondari huko Mwadui na baadae kupata uhamisho katika shule moja jijini Dar es Salaam iitwayo Dar Christian Seminary. Alivyomaliza kidato cha nne akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Jitegemee ilioko huko huko Dar es salaam.

Shughuli za uigizaji

Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya "90". Ila kufahamika zaidi alianza mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group.
Picha:Kanumba Picha.jpg
Steven Kanumba
Hivi sasa amejibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na amekuwa kipenzi cha wengi na amekubalika karibuni nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu.
Kwa sasa ameanza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria wamependezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo wameshawahi kushirikiana pamoja ikiwemo na ile ya Dar to LagosShe is My Sister na nyingine ambazo bado zinajengwa.

Maono Yake

Steven Kanumba ametangaza hivi karibuni nia ya kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Filamu na Tamthilia Alizotunga

Filamu na Tamthilia Alizoigiza

No comments: