member

Tuesday 5 November 2013

Osama bin Laden

Osama bin Laden


Osama bin Laden mnamo 2010
Osama bin Mohammed bin Awad bin Laden (Ar.: أسامة بن محمد بن عوض بن لادن‎ ʾusāmah bin muḥammad bin ʿawaḍ bin lādin); * 10 Machi 1957 – + 2 Mei 2011, alikuwa mwanzilishaji na kiongozi wa kundi la Al Qaida. Anatazamiwa na watu wengi kama gaidi aliyesababisha vifo vya watu wengi katika mashambulio ya kigaidi huku Nairobi na Dar es Salaam mwaka 1998 na hasa huko Marekani ya tarehe 11 Septemba 2001. Kuna pia wengine wanaomwona kama mteteaji wa haki za Waislamu dhidi ya mashambulio ya Marekani akitumia mbinu za jihadi. Aliuawa na wanajeshi wa Marekani tarehe 2 Mei 2011 nchini Pakistan.

Familia na kazi[hariri]

Osama bin Laden alizaliwa katika familia tajiri ya Bin Laden wa Saudia. Baada ya masomo yake kwenye chuo kikuu yasiyojulikana kama amayamaliza alifanya kazi katika makampuni ya ujenzi ya familia yake.

Afghanistan[hariri]

Tangu uvamizi wa Umoja wa Kisovyeti katika Afghanistan mwaka 1979 alikusanya pesa kwa ajili ya mujahidin wa Afghanistan akawasaidia pia vijana waarabu waliotaka kujiunga na mujahedin katika mapambano dhidi ya jeshi la Kisoveti na serikali ya Afghanistan. 1984 alihamia Pakistan kwa shabaha ya kuongoza wapiganaji wa kujitolea kutoka Uarabuni. 1986 alichukua pia wanawake na watoto zake kutoka Saudia na kwa miaka kadhaa alikaa nao Pakistan. Mwenyewe alianza kushiriki katika mashumbulio dhidi ya jeshi la Kisovyeti pamoja na vikundi vidogo vya Waarabu.

Kuanzishwa kwa Al Qaida[hariri]

Mwaka 1988 jeshi la Kisovyeti ilianza kuondoka Afghanistan. Viongozi wa mujahedin Waarabu katika Afghanistan waliokuwa Bin Laden na Wamisri kama Aiman az-Zawahiri na Abdullah Azzam walishauriana pamoja namna gani kuendeleza jitihadi zao. Walitofautiana kama kulenga serikali za nchi za Kiarabu zisizokuwa za kidini kama huko Misri au kuhamia Palestina au kupeleka jihadi yao kwenda jamhuri za Kisovyeti za Asia ya Kati kama Tajikistan au Kirgistan zilizokaliwa na Waislamu.
Mkutano huu ulifanyika katika kambi lililoitwa "al-qaida" kwa kiarabu. [1] . Hili lilikuwa baadaye jina kwa kundi lililoongozwa na bin Laden.
Sehemu ya mujahidin Waarabu walimfuata bin Ladin katika kushambulia jeshi la serikali la Afghanistan iliyoendelea kujitetea hata baada ya kuondoka kwa Wasovyeti. Mwaka bin Laden alitembelea tena Saudia akashauriana na serikali kuendelea namna gani. Alipopewa jibu heri arudi kwake akatii akarudi pamoja na kikosi chake.

Saudia 1989 - 1992 na Sudan hadi 1995[hariri]

Baada ya kurudi Saudia aliishi Madina na Jiddah akaingia tena katika kampuni ya familia yake na kusimamia miradi ya ujenzi wa barabara. Wengi walimtazama kama mshujaa aliyewajibika kwa kiasi kikubwa kufukuza Umoja wa Kisovyeti kutoka Afghanistan.
Mwaka 1990 serikali ya Saddam Hussein wa Irak ilivamia Kuwait. Serikali ya Kisaudi iliogopa mashamblio mengine dhidi ya Saudia ikakubali kufika kwa wanajeshi wa Marekani nchini. Osama aliona hatua hii kama marufuku kwa sababu aliamini Uarabuni ni nchi takatifu kutokana na mahali patakatifu pa Kiislamu pa Makka na Madina akajitolea kukusanya mujahidin 100,000 kama ulinzi dhidi ya Saddam badala ya kuwaruhusu Wamarekani. Lakini serikali ilikataa.
Wanajeshi kadhaa wa Marekani waliendelea kukaa katika Saudia hata baada ya ushindi juu ya Irak katika vita Hapo bin Laden alianza kupinga waziwazi siasa ya serikali yake. Kutokana na ugomvi huu aliamua kuhamia nchi ya Sudan alipotumia utajiri wake kuanzisha miradi, mashamba na makampuni lakini pia makambi kwa ajili ya vijana wafusi wa Uislamu mkali waliomfuata na kuhamia Sudan. Alikaa karibu na viongozi wa kundi la Al-Jihad ya Misri waliowahi kushirikiana naye Afghanistan na kupambana dhidi ya serikali ya rais Mubarak.
Kukaa kwa Wamarekani katika Saudia na kuingilia kwa Marekani katika vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia tangu Desemba 1992 kwa niaba ya Umoja wa Mataifa ilileta imani kati ya Waislamu wakali kuwa nchi za Magharibi wanaendesha vita ya misalaba mipya.
Katika miaka iliyofuata yalitokea mashambulio mbalimbali dhidi ya wanajeshi na taasisi za Kimarekani yaliyoendeshwa na wanajihadi mbalimbali kama vile huko Yemen 1992 na shambulio la 1993 dhidi ya World Trade Center mjini New York. Haijulikani hadi leo ni kiasi gani ya kwamba Osama na Al Qaida yalioshiriki katika mipango hii lakini watendaji walikuwa watu wenye mawasiliano na Bin Laden. Pia alitoa pesa kwa vita ya harakati ya kijihadi ya Groupe Islamique Armee nchini Algeria na kuhubiri dhidi ya serikali ya Saudia. Hapo Saudia ilifuta uraia wake na kukamata mali yake nchini. Familia ya bin Laden ilitangaza ya kwamba walimfukuza katika ukoo.
Mwaka 1995 wanajihadi wa Al-Jihad ya Misri walijaribu kumwua rais Mubarak wa Misri kwenye mkutano wa Umoja wa Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa. Hapo Umoja wa Mataifa ilidai Sudan kuwakabidhi kwa mahakama watendaji waliotoka huko na kutangaza hatua dhidi ya taifa hili. Sudan ilijaribu kuepukana na kuadhibiwa na jumuiya ya kimataifa haikutaka kuonekana kama msaidzi wa ugaidi ikalazimisha wanajihadi wa kimataifa kuondoka. Tarehe 18 Mei 1996 Osama bin Laden alipelekwa tena Afghanistan.

Afghanistan 1996–2001[hariri]

Afghanistan ilikuwa katika hali ya vita ya wenyewe kwa wenyewe na miezi michache baada ya kufika kwa Osama kundi la Taliban lilivamia mji mkuu wa Kabul na kutangaza Emirati ya Afghanistan likaendelea kutawala sehemu kubwa ya nchi.
Katika maeneo yaliyokuwa chini ya serikali ya Taliban Osama aliweza kuanzisha makambi mbalimbali alipopokea na kufunza wanajihadi kutoka nchi mbalimbali. Pamoja na Aiman az-Zawahiri alitoa tamko lafatwa mnamo tar. 23 Februari 1998 waliposema "Kuwaua Wamarekani na wanaoshikamana nao -kama ni wanajeshi au watu raia- ni wajibu wa kila Mwislamu mwenye uwezo wa kuyatekeleza katika nchi yoyote kwa kusudi la kuleta ukombozi wa msikiti wa al Aqsa na Masjid al-Haram (msikiti wa Makka) na kuwafukuza wanajeshi wao kutoka nchi zote za Uislamu .. Kwa msada wa Mungu tunamwita kila Mwislamu anayemwamini Mungu kutekeleza amri wa Mungu na kuwaua Wamarekani na kupora pesa zao kila mahali anapoikuta"
Mwaka uleule wa 1998 mabomu mawili yalipuliwa kwenye mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki dhidi ya balozi za Marekani huko Nairobi na Dar es Salaam yaliyoua zaidi ya watu 300 na kuwajeruhi maelfu. Serikali ya Marekani ilijaribu kuwashawishi viongozi wa Taliban kuwakabidhi bin Laden lakini hadi 2001 badi hawakufikia mapatano.
Tarehe 12 Oktoba 2000 wanajihadi wa al Qaida walishambulia maonowari USS Cole nchini Yemen. Tarehe 9 Septemba 2001 wapiganaji wa al Qaida walimwua mpinzani wa Taliban Ahmad Shah Massoudkwa bomu.
Tendo hili lilifuatwa na mashambulio ya kigaidi ya 11 Septemba 2001 katika Marekani yaliyoua takriban watu 3,000. Marekani ilidai tena Afghanitan imkabidhi bin Laden lakini viongozi wa Taliban walikataa wakadai kuonyeshwa uthebitisho. Rais Bush wa Marekani alijibu kwa kushambulia Afganistan tar. 7 Oktoba 2001; baada ya kutekwa kwa Kabul bin Laden alikimbia kwenye mipango ya milima ya Tora Borana kutoka huko katika maeneo ya Pakistan kaskazini-mashariki ambako serikali ya taifa ilikuwa na athira ndogo.
Jitihada wa Wamarekani kumkamata zilikuwa bila mafanikio. Inaaminiwa ya kwamba Osama bin Laden aliendelea kujificha nchini Pakistan, labda kwa msaada wa sehemu ya huduma ya usalama ya kijeshi ya nchi hiyo. Alitoa matagazo mbalimbali kwa njia ya kanda za video zilizosambazwa duniani kwa njia ya intaneti. Kuna dalili ya kwamba aliishi kwa siri tangu mwaka 2006 katika mji wa Abbottabad kwenye nyumba alipouawa mwaka 2011.
  1. Jump up القاعدة‎ al qaida inamaanisha "kambi" katika lugha ya Kiarabu
[[nd

No comments: