member

Friday 10 August 2012

MUHAMMAD ALI


MUHAMMAD ALI


Muhammad Ali

Muhammad Ali
Muhammad Ali NYWTS.jpg
Takwimu
JinaMuhammad Ali
Jina la kuzaliwaCassius Marcellus Clay Jr.
Jina la utaniThe Greatest, The Champ,
The Louisville Lip
Urefu1.91 m (6 ft 3 in)
Kufikia2 M
Mgawanyiko wa uzitoUzito mkubwa
UtaifaMarekani
Tarehe ya kuzaliwa17 Januari 1942 (umri 70)
Mahala pa kuzaliwaLouisville, Kentucky, U.S.
MsimamoOrthodox
Rekodi ya ndondi
Jumla ya mapigano61
Ameshinda56
Alizoshinda kwa kuangusha37
Alizopteza5
Sare0
Pambano asiloshiriki0
Muhammad Ali (amezaliwa na jina la Cassius Marcellus Clay Jr.; mnamo17 Januari1942) ni mwanamasumbwi mstaafu kutoka nchini Marekani. Amepata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu. Huyu anatazamika kama mmoja wa wanamasumbwi bora wa uzito wa juu wa muda wote. Wakati akiwa mwanamasumbwi wa ndondi za ridhaa, alishinda medali ya dhahabu ya uzito wa chini kwenye mashindano ya Olompiki ya mwaka wa 1960 yaliyofanyika mjini RomeItalia. Baada ya kuwa mwanamasumbwi wa kulipwa, amekwenda kuwa mwanandondi wa kwanza kushinda mara tatu daraja la lineal. Mnamo mwaka wa 1999, Ali alipewa taji la "Mwanamichezo wa Karne" na Sports Illustrated na "Mwanamichezo Mashuhuri wa Karne" na BBC.[1]
Anafahamika sana kwa staili ya upiganaji wake, ambapo aliielezea staili yake kuwa ni "napaa kama kipepeo, nauma kama nyuki".[2]
Awali alijulikana kama Cassius Clay, lakini alibadilisha jina lake baada ya kujiunga na jumuia ya Kiislamu ya Nation of Islam mnamo mwaka wa 1964, baadaye akabadilisha dini na kuwa Mwislamu kunako mwaka wa 1975. Mnamo mwaka wa 1967, Ali alikataa kuwekwa katika orodha ya majeshi ya Marekani kutokana na imani ya kidini na kupinga vita dhidi ya Vietnam. Alikamatwa na kupatikana na hatia juu ya rasimu ya ukwepaji mashtaka, wakamvua taji lake la uwanamasumbwi, na leseni yake ya uwanamasumbwi ikazuiliwa. Hakufungwa, lakini hakupambana kwa takriban miaka minne mpaka hapo rufaa yake ilipofanyiwa kazi na Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo akaja kushinda.

No comments: