member

Friday 6 December 2013

Benjamin Mkapa

Benjamin Mkapa

Rukia: urambazaji, tafuta
Benjamin Mkapa

Muda wa Utawala
23 November 1995 – 21 December 2005
Makamu wa Rais Omar Ali Juma (1995–2001)
Ali Mohamed Shein (2001-05)
mtangulizi Ali Hassan Mwinyi
aliyemfuata Jakaya Kikwete

Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu,
Muda wa Utawala
1992 – 1995
Rais Ali Hassan Mwinyi

Waziri wa Habari na Utangazaji
Muda wa Utawala
1990 – 1992
Rais Ali Hassan Mwinyi

tarehe ya kuzaliwa 12 Novemba 1938 (umri 75)
Ndanda, Masasi, Tanganyika
utaifa Mtanzania
chama
ndoa Anna Mkapa
watoto 2
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere
Chuo Kikuu cha Columbia
Fani yake mwandishi wa habari, mwanadiplomasia
dini Ukristo
Benjamini William Mkapa (amezaliwa 12 Novemba 1938) ni Rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995-2005) na Mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi, CCM (Revolutionary State Party).[1]

Wasifu

Mkapa ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Makerere.[1] Nafasi alizoshikilia zamani ni pamoja na kuwa afisa wa utawala huko Dodoma na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu. Yeye pia aliongoza ujumbe wa Tanzania huko Marekani na alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje kutoka 1977 hadi 1980 na kutoka 1984 hadi 1990.[2]
Katika mwaka wa 1995, Mkapa alichaguliwa rais msingi wake ukiwa kwa kampeni maarufu ya kupambana na ufisadi na kwa kumuunga mkono kwa nguvu rais wa zamani Julius Nyerere [3] Juhudi za Mkapa za kupambana na ufisadi ni pamoja na kuumba jukwaa la wazi lililoitwa Tume ya Rais juu ya Ufisadi (Tume ya Warioba) na kuongeza msaada kwa Afisi ya Kuzuia Ufisadi.[3]
Muhula wa pili wa miaka 5 wa Mkapa kama Rais uliisha Desemba 2005. Katika wakati wake ofisini, Mkapa alibinafsisha makampuni yanayomilikiwa na serikali na akaweka sera za soko huru.[4] Wafuasi wake walimtetea kuwa kuvutia uwekezaji wa kigeni ungesaidia kukuza uchumi. Sera zake zilipata msaada wa Benki ya Dunia na IMF na kupelekea baadhi ya madeni ya nje ya Tanzania kufutiliwa mbali.[3]
Amekashifiwa kwa upungufu wa baadhi ya jitihada zake za kupambana na ufisadi [3] vilevile njia yake duni ya kutumia fedha. Alitumia £15 milioni kununua ndege ya kibinafsi ya kirais, vilevile karibu £30 milioni kwa vifaa vya angani vya kijeshi ambavyo wataalam waliona yalizidi mahitaji machache ya majeshi ya nchi .[5] Ilikuwa juu ya ununuzi huu wa mwisho ndipo Katibu wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza wa wakati huo Clare Short alielezea hasira ya umma, na kusababisha yeye kujulikana kama 'Mama Radar' katika vyombo vya habari vya Tanzania.
Baada ya kutoka ofisini kutokana na kukamilisha mihula miwili inayoruhusiwa, Mkapa anakumbwa na shutuma nyingi za ufisadi kati yao kujipa mwenyewe na Waziri wake wa zamani wa nishati na madini Daniel Yona "Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira" yenye faida kubwa katika Nyanda za juu za kusini mwa Tanzania bila taratibu zifuatazo. Kwa kujibinafsishia mwenyewe mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, alivunja katiba ya Tanzania ambayo haimruhusu rais kufanya biashara yoyote katika ikulu.
Aliteuliwa katika Bodi ya Wadhamini ya Chuo cha Aga Khan mwezi Novemba 2007.[4]

Heshima na Tuzo

Nishani

Nishani Nchi Mwaka Ref
Order of the Golden Heart of Kenya.svg Nishani ya Moyo wa Dhahabu wa Kenya (Chifu) Bendera ya Kenya Kenya 2005 [6]
Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Tanzania) - ribbon bar.png Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bendera ya Tanzania Tanzania 2011

Shahada za Heshima

Chuo Kikuu Nchi Shahada ya Uzamivu Mwaka Ref
Chuo Kikuu cha Sōka Bendera ya Japani Japan Shahada ya Heshima 1998 [7]
Chuo cha Morehouse Flag of the United States.svg Marekani Shahada ya Heshima 1999 [7]
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Bendera ya Tanzania Tanzania Shahada ya Heshima 2003 [7]
Chuo Kikuu ya Kitaifa cha Lesotho Bendera ya Lesotho Lesotho Daktari wa Sheria 2005 [7]
Chuo Kikuu cha Kenyatta Bendera ya Kenya Kenya Daktari wa Elimu 2005 [8]
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bendera ya Tanzania Tanzania Shahada ya Heshima 2005 [7]
Chuo Kikuu cha Nyukasal Flag of the United Kingdom.svg Uingereza Daktari wa Sheria ya Kiraia 2007 [9]
Chuo Kikuu cha Rasi ya Pwani (Cape Coast) Bendera ya Ghana Ghana Daktari wa Barua 2008 [10]
Chuo Kikuu cha Makerere Bendera ya Uganda Uganda Daktari wa Sheria 2009 [11]

Marejeo

  1. Jump up to: 1.0 1.1 [1] ^ "Benjamin Mkapa", Microsoft Encarta Encyclopedia 2001, WGBH (FM), pbs.org, ilitolewa 19-Oktoba-2009
  2. Jump up Benjamin Mkapa,
  3. Jump up to: 3.0 3.1 3.2 3.3 [4] ^ Bruce Heilman na Laurean Ndumbaro, "Corruption, Politics and Societal Values in Tanzania: An Evaluation of the Mkapa Administration's Anti-Corruption Efforts", Afr. J. polit. sd. (2002), Toleo 1 Nambari 7
  4. Jump up to: 4.0 4.1 [10] ^ "Mheshimiwa Benjamin William Mkapa", Bodi ya Wadhamini, Chuo cha AKU, ilitolewa 19-10-2009
  5. Jump up [9] ^ Gideoni Burrows, "We sell arms to Saddam's friends", New Statesman, 8 Septemba 2003
  6. Jump up Mkapa lauds Kenya's democratic posture. panapress.com (12 October 2005). Rudishwa juu ya 26 Septemba 2013.
  7. Jump up to: 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 83RD Annual District Conference & Assembly (PDF) (Kiingereza). Page 10, Rotary International District 9200 (17 May 2008). Rudishwa juu ya 26 Septemba 2013.
  8. Jump up Prominent Alumni (Kiingereza). Kenyatta University. Rudishwa juu ya 26 Septemba 2013.
  9. Jump up Citation: Benjamin William Mkapa DCL (PDF) (Kiingereza). Newcastle University (2007). Rudishwa juu ya 26 Septemba 2013.
  10. Jump up UCC honours former Tanzanian leader (Kiingereza). Rudishwa juu ya 26 Septemba 2013.
  11. Jump up H.E. Benjamin Mkapa receives Makerere Honorary PhD (Kiingereza). Makerere University (27 November 2009). Rudishwa juu ya 26 Septemba 2013.

Viungo vya nje

Alitanguliwa na
Ali Hassan Mwinyi
Rais wa Tanzania
1995-2005
Akafuatiwa na
Jakaya Kikwete
Kigezo:Tume kwa Afrika

Viungo vya nje

Wikiquote-logo.svg
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:

No comments: